Machi 12 kama leo, mwaka jana, nilitangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli. Kabla ya tangazo langu hilo, tayari kulikuwa na tetesi kadhaa kwamba afya ya kiongozi huyo ilikuwa tete. Hata hivyo, kwa kupitia vyanzo vyangu vya kuaminika, nilikuwa mtu wa kwanza kutangaza kifo hicho. Lakini madhila yaliyonikumba baada ya kuweka taarifa hiyo hadharani, sintoyasahau. Nilitukanwa, nililaaniwa, nilitishwa, na kwa hakika laiti hao waliokerwa wangeweza kunifikia, bila shaka muda huu ningekuwa marehemu. Hatimaye, siku tano baadaye, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan alitangaza kuwa kweli Magufuli amefariki. Nami ikawa ahueni kwangu. Baadhi ya walionitukana, walikuja kuniomba msamaha japo haikusaidia kitu. Hata hivyo nafarijika kwa kuwatumikia Watanzania ipasavyo na kuwa chanzo cha kuaminika cha habari mbalimbali.
Machi 12 kama leo, mwaka jana, nilitangaza kifo cha Magufuli... kilichofuata sintokisahau maishani
Mar 11, 2022
Listen on
Substack App
Spotify
RSS Feed
Recent Episodes
Share this post