Bashite achafua hewa CCM, amrushia kijembe JK, asema "sio utaratibu kwa wastaafu kila siku kuongeaongea", amwamuru Waziri Mkuu Majaliwa kumaliza kero za ardhi ndani ya miezi 6
Kama hotuba ya Bashite wiki iliyopita ambayo ilikuwa ya kwanza tangu ateuliwa na Mama Samia kuwa mwenezi wa CCM iliwaacha baadhi ya watu wakiwa na matumaini kwamba “labda amepitiwa tu, lakini kuwekwa benchi kumembadili”, hotuba yake ya pili hapo jana bila shaka itakuwa imeondoa kabisa hisia hizo.
Kabla ya kuingia ndani zaidi, soma uchambuzi huu wa kiintelijensia kuhusu hotuba hiyo ya kwanza ya Bashite wiki iliyopita
Jasiri haachi asili: Bashite ni yuleyule, nyodo zake jana alipohutubia kwa mara ya kwanza ni ishara kuwa yajayo yanatisha, atakuwa hatari zaidi ya alivyokuwa zama za JPM
Kama kuna mtu aliamini kwamba Bashite alikuwa likizo, na kwamba kurudi kwake baada ya likizo hiyo kungemfanya mnyenyekevu, basi hotuba ya jana ya msema ovyo huyo imeondoa kabisa fikra hizo. Kuna mambo mawili ya msingi. La kwanza ni ukweli kitendo cha Mama Samia kwenda kumuibua Bashite ili ashike gurudumu la CCM kwenye uenezi ni ishara kwamba Bashite ni m…
Katika hotuba yake ya jana sio tu alithibitisha kuwa hajabadilika bali pia alionyesha bayana kuwa kuna uwezekano akawa mtu hatari zaidi ya alivyokuwa enzi za JPM, kitu ambacho Jasusi alikibashiri kwenye uchambuzi wa awali kuhusu kuteuliwa kwake.
Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu Mama Samia kumteua Makonda kuwa mwenezi CCM, ni wadhifa wa mpito tu, anaandaliwa "makubwa zaidi".
Jana Oktoba 22 ya mwaka huu 2023, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitangaza kumrejesha kada wake Paul Makonda katika medani za uongozi baada ya kumteua kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi. Uchambuzi huu wa kiintelijensia unabainisha sababu halisi zilizopelekea uteuzi huo sambamba na kudokeza kuhusu “makubwa yajayo”.
Makala hii inachambua kwa kifupi baadhi ya kauli za Bashite alizotoa jana huko Dodoma ambako alipokelewa rasmi baada ya mapokezi ya wiki iliyopita jijini Dar.