Ugaidi ni Nini? Na Magaidi ni Watu Gani Hasa? Sehemu ya Kumi na Mbili: Al-Shabaab ya Somalia, 'tawi' maarufu zaidi la Al-Qaeda
Karibu katika mfululizo wa makala kuhusu ugaidi.
Hamasa ya kuandika makala hizi imetokana na mafanikio makubwa ya kitabu cha “Afisa Usalama wa Taifa ni Mtu Gani? Na Anafanya Nini?” ambacho kilitokana na mfululizo wa makala kama huu.
Kadhalika, hivi karibuni mwandishi alichapisha kitabu kingine kilichotokana na mfululizo wa makala kuhusu "UJASUSI (espionage) ni Nini? Na MAJASUSI (spies) Wanafanya Kazi Gani Hasa?"
Kimataifa, vitabu hivi vinapatikana HAPA
Kabla ya kuingia kwenye sehemu hii ya kumi na mbili ya mfululizo wa makala hizi kuhusu ugaidi, inashauriwa kusoma sehemu ya kumi na moja ambayo ndani yake kuna links za sehemu nyingine zilizotangulia
Kama ilivyoelezwa kwenye sura zilizopita, kundi la kigaidi la Al-Qaeda lina “matawi” lukuki yaliyosambaa sehemu mbalimbali duniani. Na moja ya matawi muhimu ya Al-Qaeda ni kundi la kigaidi la Al-Shabaab la nchini Somalia.
Historia ya Al-Shabaab
Al-Shabaab, au "Vijana," ni kundi la kigaidi lenye makao yake nchini Somalia. Kundi hili linabaki kuwa mojawapo ya washirika wenye nguvu na wenye mafanikio zaidi wa al-Qaeda.