Ugaidi ni Nini? Na Magaidi ni Watu Gani Hasa? Sehemu ya Kumi na Moja: Matawi Lukuki ya al-Qaeda
Karibu katika mfululizo wa makala kuhusu ugaidi.
Hamasa ya kuandika makala hizi imetokana na mafanikio makubwa ya kitabu cha “Afisa Usalama wa Taifa ni Mtu Gani? Na Anafanya Nini?” ambacho kilitokana na mfululizo wa makala kama huu.
Kadhalika, hivi karibuni mwandishi alichapisha kitabu kingine kilichotokana na mfululizo wa makala kuhusu "UJASUSI (espionage) ni Nini? Na MAJASUSI (spies) Wanafanya Kazi Gani Hasa?"
Kimataifa, vitabu hivi vinapatikana HAPA
Kabla ya kuingia kwenye sehemu hii ya kumi na moja ya mfululizo wa makala hizi kuhusu ugaidi, inashauriwa kusoma sehemu ya kumi ambayo ndano yake kuna links za sehemu nyingine zilizotangulia
Tangu kuundwa rasmi kwa kundi la al-Qaida, kulikuwa na mkazo kwenye kulifanya kundi hilo liwe mtandao mpana badala ya kundi moja pekee. Ni kwa mantiki hiyo, baada ya Marekani kutangaza vita ya kimataifa dhidi ya ugaidi huku mlengwa mkuu akiwa kiongozi wa al-Qaeda Osama bin Laden na kundi hilo kwa ujumla, baadhi ya wanataaluma wa stadi za ugaidi walihoji kama vita hiyo ingekuwa na ufanisi, kwani adui hakuwa mtu mmoja au kundi moja bali itikadi zaidi.
Na japo vita hivyo ilifanikiwa kupunguza nguvu za “al-Qaeda kuu”, kundi hilo la kigaidi lilifanikiwa kusambaa katika maeneo mbalimbali duniani ambako matawi yake yameendelea kuwa tishio.
Makala hii inayatambulisha baadhi ya matawi maarufu ya al-Qaeda. Hata hivyo, kama ilivyoelezwa katika sura za mwanzo, ugaidi ni kitu kinachobadilika mara kwa mara, matawi ya al-Qaeda yanavyobadilika mara kwa mara