Barua Ya Chahali

Share this post
Uchaguzi TLS: Ushindi wa Prof Hosseah unaashiria kuporomoka kwa nguvu ya ushawishi wa Chadema, waliweza kumuingiza madarakani 2021 wameshindwa kumzuwia asirudi madarakani 2022
www.baruayachahali.com

Uchaguzi TLS: Ushindi wa Prof Hosseah unaashiria kuporomoka kwa nguvu ya ushawishi wa Chadema, waliweza kumuingiza madarakani 2021 wameshindwa kumzuwia asirudi madarakani 2022

Evarist Chahali
May 28
4
Share this post
Uchaguzi TLS: Ushindi wa Prof Hosseah unaashiria kuporomoka kwa nguvu ya ushawishi wa Chadema, waliweza kumuingiza madarakani 2021 wameshindwa kumzuwia asirudi madarakani 2022
www.baruayachahali.com

Kwanza Jasusi anaomba ajipongeze kwa kubashiri kuwa Profesa Edward Hosseah angeshinda kinyang’anyiro cha urais wa TLS uliofanyika jana huko Arusha.

Read Barua Ya Chahali in the new Substack app
Now available for iOS

Katika makala hii iliyochambua kuhusu uchaguzi huo, Jasusi alitanabaisha haya pichani

Unaweza kusoma makala nzima hapa chini

Barua Ya Chahali
Siasa "zilivyopora" uchaguzi wa TLS ni kiashiria cha jinsi taaluma ya uanasheria inavyofeli katika utumishi kwa Watanzania hususan "wasio na vyama."
Moja ya taaluma ambazo Jasusi alikuwa anaziheshimu sana kwa Tanzania ni uanasheria. Na heshima hiyo ilianzia chuo kikuu cha Dar es Salaam ambako Jasusi alisomea shahada yake ya kwanza. Pale UDSM, wanafunzi wa sheria walikuwa na “mwonekano” tofauti na sie wanafunzi wengine. Kimsingi hata jengo la kitivo chao lilikuwa na mwonekano tofauti…
Read more
2 months ago · 4 likes · Evarist Chahali

Baada ya kijpongeza huko (kuna busara zinasema “jipongeze mwenyewe au subiri milele kupongezwa”, ambao unaakisi Tanzania yetu yenye watu wepesi kukosoa lakini wagumu kupongeza, isipokuwa kwenye UBUYU 😡), jasusi anatupia jicho tafsiri pana ya ushindi wa Profesa Hosseah na kampeni kubwa za wafuasi wa Chadema kumzuwia asirudi madarakani.

Ndoa ya Chadema na Profesa Hosseah

Katika uchaguzi wa TLS mwaka jana, viongozi kadhaa waandamizi wa Chadema pamoja na lundo la wanachama wa kawaida wa chama hicho walifanya jitihada kubwa za kumpigia kampeni Profesa Hosseah ambaye kwa wakati huo alikuwa bado Dokta Hosseah.

Share Barua Ya Chahali

Japo haijawekwa wazi kwanini chama hicho kilimpigia kampeni bosi huyo wa zamani wa TAKUKURU, taarifa zinadai kuwa ni “masuala ya binafsi” zaidi.

Na jitihada zao zilizaa matunda ambapo mgombea huo alishinda kwa kishindo.

Jasusi hakupendezwa

Jasusi alikuwa miongoni mwa waliokwazwa na kitendo hicho cha wana-Chadema hao, kwa sababu kuu tatu. Kwanza, jasusi alihofia kuwa kwa wana-Chadema hao kumsapoti “mgombea wao” huko TLS, kuna hatari kwa vyama vingine - hususan chama tawala CCM - kuiga mkumbo, na matokeo yake uchaguzi wa taasisi hiyo muhimu itageuka ya kikada zaidi kuliko ya kitaalamu.

Sababu ya pili ni ukweli kwamba rekodi ya mgombea huyo haikuwa ya kuvutia. Jasusi alijaribu kukumbushia lundo la skandali za rushwa lililogubika utawala wa mgombea huyo alipokuwa mkuu wa taasisi ya kupambana na rushwa. Kadhalika, baadhi ya viongozi wa Chadema walikuwa mstari wa mbele kutana mgombea huyo awajibishwe alipokuwa bosi wa TAKUKURU kwa madai ya kushindwa kazi. Hoja ya jasusi ilikuwa simpo: kama aliboronga huko nyuma, iweje sasa ageuke “malaika” wa kupigiwa kampeni?

Barua Ya Chahali
Dear Mama @SuluhuSamia, mabalozi hawa wawili wanakuhujumu
Inatanabaishwa kuwa moja ya dhambi kuu kwenye taaluma ya intelijensia ni kushindwa kutahadharisha. Hii inachangiwa na ukweli kwamba taaluma hiyo inatarajiwa zaidi kubaini matishio ya kiusalama kabla hayajasababisha madhara. Makala hii ya kiintelijensia inaeleza kuhusu hujuma za mabalozi wawili wa Tanzania wanavyomhujumu Rais Samia Suluhu pamoja na Tanzania kwa ujumla…
Read more
2 months ago · 1 like · Evarist Chahali

Kama kawaida, badala ya hoja za jasusi kujibiwa, aliishia kunyeshewa mvua ya matusi.

Sababu ya tatu, na hii ni ya msingi zaidi, moja ya vitu vinavyokwaza demokrasia nchini Tanzania ni siasa kuingizwa kwenye taasisi za kitaalamu, huku mfano maarufu ukiwa ni wa Idara ya Usalama wa Taifa. Kwa kuruhusu siasa ziingilie masuala binafsi ya TLS, kama uchaguzi mkuu, kinachofanyika ni kilekile cha TISS kuacha kushughulikia usalama wa taifa na kujiingiza kwenye masuala ya siasa. Matokeo yake sote twayajua.

Kuvunjika kwa ndoa ya Chadema na Prof Hosseah

Chanzo ni udikteta. Kwamba Profesa Hosseah alitarajiwa afanye kazi zake kwa matakwa ya Chadema. Na kubwa ni suala la Katiba Mpya ambalo chama hicho limebinafsishwa na chama hicho.

Kitendo cha Profesa Hosseah kama Rais wa TLS kukubali kuwa mjumbe wa kikosi kazi cha Rais kuhusu masuala ya siasa, kilitosha kuwafanya wana-Chadema wamuone mwanasheria huyo kuwa ni msaliti, na wakaamua kuwaunga mkono wapinzani wake katika nafasi ya urais wa taasisi hiyo.

Kilichowapa jeuri wana-Chadema hao ni imani fyongo kwamba kwa vile waliweza kumuingiza madarakani Profesa Hosseah katika uchaguzi uliopita kwa kampeni yao kubwa, basi hata wakati huu wangeweza kumzuwia “kwa ushawishi walionao.”

Read Barua Ya Chahali in the new Substack app
Now available for iOS

Matokeo yamekuwa kinyume na matarajio yao.

Kwanini wamefeli kumzuwia Profesa Hosseah?

Kuna sababu kadhaa lakini za msingi ni kama ifuatavyo.

  • Profesa Hosseah kama mgombea aliyekuwa anatetea nafasi yake alikuwa na nafasi nzuri zaidi wa wapinzani wake. Katika chaguzi zote, mgombea anayewania kubaki madarakani anakuwa na faida kadhaa, ikiwa ni pamoja na “nimefanya hili na lile” ilhali wapinzani wake wanaishia kuahidi tu “nitafanya hili na lile.”

  • Kwa Profesa Hosseah uchaguzi huo ulikuwa kile Waingereza wanaita “his to lose” yaani kwa lugha ya mtaani “yeye na nyavu, ashindwe yeye tu”, kwamba ingetokea miujiza akashindwa, basi isingekuwa kutokana na uimara wa wapinzani wake bali uzembe wake.

  • Uamuzi wa wana-Chadema kuwaunga mkono wapinzani wa Profesa Hosseah ulisaidia tu kugawa kura za wagombea hao huku wakimnufaisha Profesa Hosseah.

  • Kwa wana-Chadema kujitokeza kumpinga hadharani, wana-CCM nao wakajiingiza kwenye kinyang’anyiro hicho, na wakapiga kampeni ya nguvu kuhakikisha Profesa Hosseah anabaki madarakani. Kwa vile CCM walikuwa wakimsapoti mgombea huyo, sintoshangaa kusikia kuwa “kitengo” pia kilitia timu Arusha kuhakikisha mgombea huyo anashinda.

Ushawishi wa Chadema umepungua?

Hilo lipo wazi. Lakini sio tu haliwasumbua wahusika bali ndio kwanza linawaongezea hasira za “kummwagia matusi kila anayekatiza kwenye anga zao.”

Ushawishi wa chama hicho unapungua kutokana na kuendekeza siasa za chuki na matusi. Idadi kubwa tu ya Watanzania haipendezwi na kasumba hiyo ambayo kimsingi inakinzana na hata utamaduni wa Chadema yenyewe.

Share

Kinachochangia matusi miongoni mwa wafuasi wa chama hicho ni ukweli kwamba wengi wao wanatumia akaunti feki. Unaweza kuthibitisha hili wewe mwenyewe leo, nenda kwenye twiti ya mwana-Chadema maarufu, yenye comments na likes kadhaa, kisha pitia profiles za walio-comment/ku-like, kisha jiridhishe wangapi ni “watu halisi” na wangapi ni wenye akaunti feki.

Echo chamber

Kuna tatizo zaidi ya hilo la kwanza, nalo ni kile Waingereza wanaita “echo chamber.” Msamiati huu unamaanisha “kusikiana wenyewe kwa wenyewe.” Ni kama vile mwangwi unavyofanya kazi, unapiga kelele kisha unajisikia mwenyewe.

Ukiangalia harakati za kisiasa za Chadema, zimejikita zaidi kwa wafuasi wake badala ya Watanzania kwa ujumla. Na mitandaoni ni hivyohivyo, nafasi ya mawazo mbadala haipo na badala yake wanajazana upepo wenyewe kwa wenyewe.

Athari za “echo chamber” ni kwamba hakuna fursa ya kujikerekebisha kwa sababu ni kama “kipofu anamuongoza kipofu mwenzie.”

Hitimisho:

Sitarajii wana-Chadema kupata funzo lolote kwenye kufeli kwao katika jitihada za kumkwamisha Profesa Hosseah. Kama ilivyo kawaida yao, pindi likitokea jambo kinyume na matarajio yao, hujifanya kama hawajalisikia. Na ndivyo walivyopokea matokeo ya uchaguzi wa TLS, wamejifanya kama hawajayasikia au hakuna kilichotokea.

Hata hivyo, mtu anayejikwaa na kupuuzia kuangalia alipojikwaa, anaweza kujikwaa tena. Wana-Chadema wakiamua kutojifunza kutokana na uchaguzi huo wa TLS, wanaweza kurudia makosa hayohayo huko mbeleni.

Wikiendi njema

Share this post
Uchaguzi TLS: Ushindi wa Prof Hosseah unaashiria kuporomoka kwa nguvu ya ushawishi wa Chadema, waliweza kumuingiza madarakani 2021 wameshindwa kumzuwia asirudi madarakani 2022
www.baruayachahali.com
TopNewCommunity

No posts

Ready for more?

© 2022 Evarist Chahali
Privacy ∙ Terms ∙ Collection notice
Publish on Substack Get the app
Substack is the home for great writing