TEKLA, a love story: Riwaya nyingine kutoka kwa Jasusi...japo hii si ya kijasusi ๐[Sehemu ya Ishirini na Mbili - Nakuja Uingereza"]
Karibuni kwenye riwaya nyingine kutoka kwa Jasusi baada ya ile ya kwanza ya โMtandaoโ ambayo wengi wenu mmeipokea vizuri. Asanteni sana.
โTekla - a love storyโ ni stori ya kutunga kama ilivyo hiyo ya kijasusi ya โMtandao.โ Kwa vile lengo la Jasusi ni kukuletea simulizi ambazo ukisoma utajisikia kama unaangalia filamu, ni rahisi kudhani kuwa yanayoongelewa ni matukio ya kweli.
Kabla ya kuingia sehemu hii ya ishirini ya riwaya hii ya kimahaba, ni vema ukijikumbusha sehemu zilizopita ambazo kwa pamoja zipo katika makala hii
Usiku wa mahaba mazito kutoka kwa Mariam ulipaswa kufanya James awe mwenye furaha tele. Lakini alipoamka huku Mariam amelala pembeni yake, aliangalia simu yake na kubaini kwamba Tekla hakupiga simu, kinyume na alivyoahidi.
James alikwenda kwenye albamu ya picha kwenye simu yake ambako kulikuwa na picha lukuki za Tekla. Alizipitia picha kadhaa za mrembo huyo, kisha akahamishia macho yake kwa Mariam. Alikuwa anajaribu kuwalinganisha mabinti hao wawili.