TEKLA, a love story: Riwaya nyingine kutoka kwa Jasusi...japo hii si ya kijasusi 😊[Sehemu ya Kumi na Tisa - "Mariam Wangu"]
Karibuni kwenye riwaya nyingine kutoka kwa Jasusi baada ya ile ya kwanza ya “Mtandao” ambayo wengi wenu mmeipokea vizuri. Asanteni sana.
“Tekla - a love story” ni stori ya kutunga kama ilivyo hiyo ya kijasusi ya “Mtandao.” Kwa vile lengo la Jasusi ni kukuletea simulizi ambazo ukisoma utajisikia kama unaangalia filamu, ni rahisi kudhani kuwa yanayoongelewa ni matukio ya kweli.
Kabla ya kuingia sehemu hii ya kumi na tisa ya riwaya hii ya kimahaba, ni vema ukijikumbusha sehemu zilizopita ambazo kwa pamoja zipo katika makala hii
TANGAZO
Kwa walio nje ya Tanzania, vitabu vinapatikana HAPA
Safari ya kwenda Dar ilikuwa ndefu sana kwa James. Kwa upande mmoja, safari hiyo ilikuwa ni ya kwanza kabisa tangu mama yake afariki na kuzikwa huko kijijini.
Kwa upande mwingine, ilikuwa ni kama anakwenda kukutana na Tekla upya, kwa maana ya kwamba, kwa muda mwingi walipokuwa wote Dar, mama yake James alikuwa bado haijapo alikuwa mahututi.
James aliwaza kama Tekla ataendelea kumpa upendo kama ule aliompatia wakati mama yake anaumwa. Aliwahi kusikia kwamba watu wenye upendo huweza kubadilika pindi kile kilichowafanya wampe upendo mtu kikiondoka.
Basi lilipofika Mikumi, James aliteremka ili kwend akupata chakula maana alikuwa anasikia njaa. Lakini kitendo cha kuteremka hapo kilimrejeshea kumbukumbu za siku ambapo yeye na Tekla na akina Ticha walikuwa wakienda kijijini kwenye msiba. Alijisikia majonzi makubwa lakini akajikaza kiume.
“Kaka pole na msiba”, ilisikika sauti ya kike nyuma ya James.