Mbinu za kijasusi unazoweza kuzitumia katika maisha ya kila siku: mbinu ya tatu - jinsi ya kugundua kama mwenza "anachepuka" [sehemu ya pili - kumfanya mchepukaji akiri mwenyewe]
ANGALIZO: Kwa watumiaji wa Gmail, endapo baruapepe haionyeshi makala nzima, basi bonyeza palipoandikwa “view entire message” mwishoni mwa baruapepe yako
Huu ni mwendelezo wa mfululizo wa makala zitakazokufahamisha mbinu mbalimbali za kijasusi/kishushushu/kiintelijensia unazoweza kuzitumia katika maisha yako ya kila siku.
Makala hii ni ya nne katika mfululizo huu. Endapo hukubahatika kusoma makala tatu zilizopita, soma hapa
Makala hii ni sehemu ya pili ya mbinu ya tatu yaani jinsi ya kugundua kama mwenza wako anakusaliti, au “anachepuka” kama wasemavyo mtaani.
Katika sehemu ya kwanza, mbinu iliyoongelewa ni intelijensia ya mwenendo wa maisha, kwa kimombo wanaita “pattern-of-life intelligence”.
Mbinu ya pili
Mbinu ya pili ina tafsiri nyingi kwa Kiswahili, ila kiintelijensia kwa kimombo ni ELICITATION. Mbinu hii itakuwezesha kupata ukweli kutoka kwa mwenza wako kwa hiari yake mwenyewe.