Kama Jasusi alivyobashiri Juni 2021 (na akaishia kutukanwa), uswahiba kati ya Chadema na mwanaharakati Maria Sarungi wavunjika
Mara zote Jasusi huwa mbele ya muda. Huyaona yajayo kabla hayajatokea. Na tukio moja kati ya mengi aliyowahi kuyabashiri kwa usahihi ni hili lililojiri punde ambapo uswahiba kati ya Chadema na mwanaharakati Maria Sarungi umevunjika.
Ili kuelewa kilichotokea, rejea makala hii ya Jasusi ya Juni 4, 2021
Uswahiba Wa Chadema Na "Wanaharakati wa Mtandaoni" Na Mustakabali Wa Chama Hicho
·
Nianze makala hii kwa kutanabaisha mapema kwamba mimi sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa tangu mwaka 1995 nilipojiunga na utumishi serikalini. Kuanzia hapo sheria ilinikataza kujihusisha na siasa isipokuwa pale tu majukumu ya kikazi yalihitaji iwe hivyo.