Heri ya mwaka mpya 2025. Jasusi anauanza kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kabisa kutengeneza albam yenye nyimbo 15 kwa kutumia akili mnemba
Heri ya mwaka mpya wa 2025. Na uwe wa heri.
#Jasusi anaanza mwaka huu kwa kuandika historia ya kipekee kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kabisa kutengeneza albamu yenye nyimbo 15 ambazo zote amezitengeneza kwa kutumia akili mnemba.
Track listing
01. Jasusi: Intro
02. Living in the Shadows
03. Mama Ndubwi
04. I'm in Love with a Professor
05. Kijani Kamanda Zambarau
06. Wadada wa Kichagga
07. Jasusi in the Middle
08. Ndoto Yangu
09. A Tanzanian in Scotland
10. Ifoza Ndio Home
11. Shoutout to Mohammed "Mo" Dewji
12. Nirapu Vipi
13. Asante Mungu
14. Tupendane
15. Jasusi: Outro
Albamu itapatikana kwenye platforms zote za muziki mtandaoni baadaye mwezi huu. Mtafahamishwa.
Unaweza kusikia vionjo kwenye ukurasa wa Instagram wa Jasusi
Japo kuna albamu nyingine ipo jikoni, haimaanishi kuwa Jasusi amevamia fani ya muziki. Lengo kuu la Jasusi katika kutengeneza albamu hii ni kuleta mwamko (awareness) kuhusu akili mnemba, ikiwa ni pamoja na faida zake lukuki lakini pia hatari zake.
Faida ni nyingi mno - kama hii ya mtu asiyejua lolote kuhusu muziki kuweza kutengeneza sio wimbo mmoja tu bali albamu nzima yenye nyimbo 15.
The future is akili mnemba. Na ni kwa muktadha huu, Jasusi anajitangaza leo 01/01/2025 kuwa "AI Evangelist" yaani "Mhubiri wa akili mnemba".
MENGINEYO
Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu Mbowe kuamua kugombea tena uenyekiti Chadema, "mpambano" wake vs Lissu, na mustakabali wa chama chao
Jana Disemba 21, 2024, inaweza kuingia kwenye kumbukumbu za historia ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kutangaza kuwa nae anawania nafasi hiyo, ambayo Makamu wake Bara, Tundu Lissu alitangaza awali kuiwania pia.