Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu Mbowe kuamua kugombea tena uenyekiti Chadema, "mpambano" wake vs Lissu, na mustakabali wa chama chao
Jana Disemba 21, 2024, inaweza kuingia kwenye kumbukumbu za historia ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kutangaza kuwa nae anawania nafasi hiyo, ambayo Makamu wake Bara, Tundu Lissu alitangaza awali kuiwania pia.
Siku hii inaweza kuingia kwenye kumbukumbu kwa sababu katika kwa zaidi ya miaka 20 ya chama hicho kikuu cha upinzani (kwa idadi ya wanachama) hakijawahi kujikuta katika hali hii ya mwenyekiti kuchuana na makamu wake kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa katika mfumo wa uongozi wa chama hicho.
Pamoja na mambo mengine, uchambuzi huu wa kiintelijensia unajikita katika
Sababu ambazo japo Mbowe hakuzitaja lakini zimechangia yeye kuchukua uamuzi huo.
Mpambano kati yake na Lissu.
Mustakabali wa Mbowe katika siasa ndani ya Chadema, Upinzani na Tanzania kwa ujumla.
Mpambano kati ya Mbowe vs Lissu na matokeo tarajiwa.
Mustakabali wa Chadema.