Zuio La Bashite Kuingia USA: Wadau Kadhaa Wanaafiki Mtazamo Wangu Kuwa Mlengwa Ni Jiwe

Nimekutana na mabandiko mawili huko Jamii Forums ambayo yanaakisi nilichoeleza katika uchambuzi wangu hapo juzi kuhusu hatua ya Marekani kumpiga marufuku Bashite kuingia nchini humo, kutokana na kuhusika kwake katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Kwa upande mwingine, “profesa aliyeokotwa jalalani ameruka kimanga taarifa ya awali iliyomnukuu akiichimbia mkwara Marekani

Taarifa ya awali ni hii

Na mtumishi wako sikuchelewa kumtafsiria Secretary Pompeo (Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani)

Mambo ni mengi lakini muda ni mchache. However, mtumishi wako ninaahidi kukuletea kila latest inayojiri kuhusu suala hili.

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali