Waraka wa PASAKA Kutoka Kijarida cha BARUA YA CHAHALI: Kwenu Vijana wa Ovyo, Lini 'Mtafufuka' Kama Bwana Yesu?
Hali Halisi ya Kizazi Kilichopotea
Katika hali ya kawaida, Pasaka ni kipindi cha tafakari kuu kwa Wakristo na wasio Wakristo pia—kipindi cha kutafakari maana ya mateso, kifo, na ufufuko wa Yesu Kristo. Huu ni wakati ambapo maisha mapya yanahimizwa, msamaha unatafutwa, na mwelekeo mpya unazingatiwa. Lakini tunapoyaona maisha ya baadhi ya vijana wetu wa sa…