Wanasema 'historia huandikwa wakati watu wanaangalia kwingineko': Hongera Mh @Nnauye_Nape kwa kuiingiza Tanzania katika mfumo wa kimataifa wa anuani za makazi (postcode). Faida ni kubwa kuliko gharama
Huenda makala hii fupi ikawakera watu wengi. Na sintoshangaa makala hii ikazua hisia kuwa “Jasusi kanunuliwa”. Tumefika mahala ambapo huwezi kupongeza jema la serikali hata kama lipo wazi bila kutuhumiwa kuwa “unataka u-DC.”
Kilichonisukuma kuandika makala hii ya pongezi kwa Mheshimiwa Nape ni taarifa nilizopata kuhusu historia inayoandikwa nchini Tanza…