Wamasai Ngorongoro wameonyesha jinsi ya kukabiliana na udhalimu, pia wamewajengea Wapinzani kesi nzito ya kihistoria kuing'oa CCM mwakani
Yaliyojiri huko Ngorongoro yanasikitisha sana. Kwamba serikali iliamua kusitisha huduma muhimu za kijamii kama afya na elimu ili kuwashinikiza Wamasai kuondoka katika makazi yao - ili makazi hayo wapewe Waarabu - ni jambo lisilo na hata chembe ya ubinadamu.
Hata hivyo, pamoja na machungu yote yanayohusiana na suala hilo, kwa namna ya kipekee, jamii ya Wamasai sio tu imemudu kufanya kile ambavyo vyaa vya upinzani vimekuwa vikisuasua kufanya, yaani kusimama kidete dhidi ya ukandamizwaji wa haki zao unaofanywa na serikali ya CCM kwa kutumia vyombo vyake vya dola, bali pia Wamasai wameweza pia kujenga kesi kubwa na ya kihistoria dhidi ya CCM.
TANGAZO
Na kesi yenyewe ni ya wazi: