Wakati Mama @SuluhuSamia anasema kuna mtandao wa wizi wa fedha za serikali, Waziri wake wa Fedha (Mwigulu) adai hakuna wizi serikalini, Waziri Mchengerwa adai huo ni wizi wa "zama za JPM" 🤔
Wakati Mama Samia Suluhu atatimiza miaka mitatu ya urais siku chache zijazo, jambo moja ambalo kila anayempenda hatosita kumshauri ni kwamba asiruhusu watendaji wake - hususan mawaziri - wamkosee heshima - hususan hadharani.
Kwa sababu, katika mantiki ya kawaida tu, kama Rais anasema kwamba kuna mfumo wa wizi wa fedha za serikali, lakini waziri wake wa f…