Wakati Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris anawasili leo Tanzania, huenda macho ya wengi yakaelekezwa kwa ulinzi wake wa "kufa mtu." Fahamu kwa kina kuhusu walinzi wake, US Secret Service.
Wakati Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, anawasili leo nchini Tanzania akitokea Ghana,
huenda macho ya wengi yataelekezwa kwa “ulinzi wake mkubwa”.
Japo Makamu wa Rais wa Marekani ni mmoja wa binadamu wanaolindwa mno duniani, ukweli kwamba Harris, ni Mmarekani Mweusi, unafanya ulinzi wake kuwa na msisitizo zaidi.
Makala hii inakueleza kwa kina kuhusu ulinzi wa kiongozi huyo anavyolindwa na kikosi cha ulinzi wa viongozi wa Marekani kinachofahamika kama the United States Secret Service, kwa kifupi USSS, almaarufu Secret Service.
Jina la msimbo (code name) la Harris linalotumiwa na Secret Service ni “pioneer”.
Kadhalika, makala inaeleza kuhusu jinsi gani maafisa wa Secret Service wanavyojiriwa na mafunzo yao yalivyo, sambamba na majukumu yao mengine licha ya ulinzi wa viongozi.
Vilevile, makala inakuonyesha tofauti baadhi ya tofauti za msingi zilizopo kati ya taasisi hiyo na kikosi cha ulinzi wa viongozi wa Tanzania kilicho ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa, kinachoitwa PSU.