Wakati kuna mashehe Arusha wapo ndani tangu mwaka 2014 kwa tuhuma za ugaidi, Waislam zaidi ya 100 wanakabiliwa na mashataka hayo Dar, Tanga, Mtwara na Morogoro; Sheikh Ponda ataka haki itendeke
Mwanaharakati wa haki za binadamu na mtetezi wa haki za Waislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda ameeleza kuwa kuna lundo la kesi za ugaidi zilizofunguliwa dhidi ya Waislamu zaidi ya 100 katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Tanga, Mtwara na Morogoro.