Wadau Hawa Wanahitaji Msaada Wako

Niliwaomba Majuzi Kuwasumbua Kuhusu Maombi Ya Wadau Mablimbali Wanaohitaji Msaada Wenu

Majuzi niliwaomba ruhusa ya kuwasumbua kwa kuwaletea maombi ya wadau mbalimbali wenye mahitaji mbalimbali. Naamini katika mkusanyiko huu wa zaidi ya watu 2,000 kuna lundo la wasamaria wema wanaoweza kuwasaidia wenzetu wenye mahitaji mbalimbali.

Utaratibu ni kwamba nitaweka screenshot za maelezo yao wenyewe ili nisiongeze au kupunguza kitu japo kuna wakati nitalazima kuhariri endapo kuna taarifa binafsi za mdau husika.

Endapo uwezo unakuruhusu na/au nafsi inakutuma kusaidia, utawasiliana nami kwa baruapepe kisha nitakuunganisha na mdau husika.

Tuna wadau watatu, wawili wanahitaji msaada wa kuwezeshwa kupata kazi, na mmoja anahitaji msaada wa ushauri wa biashara

Mdau mwingine huyu hapa chini

Na mwisho kwa sasa ni mdau huyu anayehitaji msaada wa ushauri wa kibiashara

Ukiwa tayari kusaidia basi wasiliana nami kwa KUBONYEZA HAPA

Naomba tu kuwahakikishia kuwa huwa ninajiridhisha kwanza kabla ya kuweka matangazo kama haya.

Kingine, moja ya tuzo kubwa kabisa katika maisha yetu ni kujibidiisha kuwasaidia wenzetu wenye mahitaji mbalimbali. Hii ni sala/dua muhimu kabisa, na ukiizowea kama mie mtumishi wako, utakuwa na amni kubwa nafsini.

Ndimi mtumishi wako Evarist Chahali