"Waarabu" wasaini mkataba na JWTZ
Kundi la EDGE la Umoja wa Falme za Kiarabu limesaini makubaliano ya ushirikiano na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa maonyesho ya ulinzi ya IDEX yanayoendelea Abu Dhabi.
EDGE ilisema makubaliano hayo, yaliyotiwa saini tarehe 21 Februari, "yatafungua njia ya ushirikiano kati ya EDGE na TPDF kuhusu fursa za kimkakati za manufaa ya pa…