#UziwaTwita Kuikaribisha Julai Na Neno Kuhusu #Uchaguzi2020

Kwanza, nina furaha kuwajulisha kuhusu ujio wa jarida la mtandaoni la JASUSI ambalo litajikita zaidi kuhusu masuala ya intelijensia. Vilevile litagusia masuala ya usalama wako mtandaoni na kukufundisha mbinu mbalimbali za kuwa salama. Kupitia jarida hilo natarajia pia kuendesha kozi ya awali ya udukuzi wa kimaadili. Nitawaletea maelezo zaidi hivi punde.

Awali niliomba maoni huko Twitter kuhusu jina la tovuti itakayobeba jarida hilo.

Pia nina furaha kuwafahamisha kuwa vitabu vyangu sasa vinauzwa kwa SHILINGI YA TANZANIA badala ya awali ambapo bei ilikuwa kwenye paundi ya Uingereza.

Anza Julai hii vema kwa kijipatia kopi yako HAPA

Niende kwenye #UziWaTwita. Bingirika nao hapa

Ndimi jasusi wako,

Evarist Chahali