Utumishi Bora Ni Pamoja na Usikivu + Kushaurika

Wadau kadhaa wamenitumia ujumbe kueleza nia yao ya kujiunga na uanachama wa #BaruaYaChahali yenye vijarida vitano kwa wiki lakini deadline ya leo imefika huku hali zao kiuchumi sio nzuri, sababu kuu moja ikiwa hawajapata mshahara.

Sasa kwa vile wazo zima la kuchangia uanachama halikuwa na malengo ya kutengeneza faida, nadhani itakuwa vema kutoa wiki mbili zaidi kwa ajili ya wote wanaotamani kuwa wanachama lakini bado hawajapata mshahara.

Kwa vile mtumishi wenu ni msikivu na anashaurika, basi naomba kutangaza kusogeza deadline ya mchango wa uanachama hadi tarehe 14.07.2019 wiki mbili kamili kutoka kesho. Sidhani kama kuna mtumishi ambaye hadi muda huo atakuwa hajalipwa mshahara.

Japo nimesikia ushauri na kuufanyia kazi, nawaomba wahusika wasifanye mzaha.

Utaratibu ni uleule kama ulivyo hapa pichani chini

Na kwa walio nje ya Tanzania, mnaweza kuchangia kwa KUBONYEZA HAPA.

Ndimi mtumishi wenu

Evarist Chahali