Utata wa Kifo Cha Sheikh Bura: Yasemekana "Alitoka Kwenye Mkutano wa ex-CAG Prof Assad"

Katika zama hizi za #WatuWasiojulikana ni muhimu kuangalia kila tukio kwa jicho la tatu. Na katika hili, naomba kukiri kwamba hata niliposikia taarifa ya kifo cha mfanyabiashara maarufu Ali Mufuruki nafsi ilihisi “huenda kuna mkono wa mtu.”

Na majuzi nilipokutana na habari ya kifo cha Sheikh Rashid Bura, hisia zangu zilipelekea kudhani huenda kuna mkono wa mtu.

Kwa mujibu wa taarifa, licha ya kuwa mmiliki wa shule ya Zam Zam mkoani Dodoma, Sheikh huyo alikuwa MWANAHARAKATI MTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU.

Kinachoweza kuchangia hisia kuwa huenda “kuna mkono wa mtu” ni jinsi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Giles Muroto alivyojikanganya katika maelezo yake kuhusu kifo hicho.

Lakini maelezo ya afande huyo yanakinzana na ya wanafamilia ambao wanaeleza kuwa mwili wa marehemu ulikutwa na majeraha.

Hata kama mwili usingekuwa na majeraha, kamanda huyo sio daktari kitaaluma kiasi cha kujipa jukumu la kutangaza kuwa marehemu alifariki kwa ugonjwa wa moyo.

Ni rahisi kuhisi kuwa kukurupuka huko sio kwa bahati mbaya bali kumelenga kuficha ukweli kuhusu kifo hicho.

Lakini taarifa mpya iliyowekwa na mwanahabari mkongwe Pascal Mayala huko Jamii Forums kuwa marehemu alihudhuria mkutano ambao pia ulihudhuriwa na CAG wa zamani, Prof Assad, inazua hisia hasi kutokana na mazingira ya hivi karibuni kuhusiana na CAG huyo wa zamani.

Kifo ni kazi ya Mungu lakini katika zama hizi za #WatuWasiojulikana, yayumkinika kuhisi baadhi ya vifo ni kazi ya shetani inayotekelezwa na hao “wasiojulikana.

Unaweza kusoma kwa kirefu kuhusu kifo cha Sheikh huyo HAPA.

Nimalizie na tangazo la vitabu

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali