Ushauri wa kiintelijensia kwa Chadema kuhusiana na maandamano yao ya Septemba 23.
Moja ya vitu vinavyomkera Jasusi ni pale anapoona analazimika kuwapatia msaada watu wasioona umuhimu wa msaada husika. Kwa mfano, wiki iliyopita, Jasusi alimfahamisha mbunge wa zamani wa chama hicho, Godbless Lema, kuhusu taarifa kwamba kuna mpango wa kumdhuru yeye na wenzie wawili.
Licha ya kum-tag, mbunge huyo wa zamani hakuona umuhimu wa angalau kuwasilian Jasusi kuhusiana na taarifa hizo.
Kadhalika, mara baada ya kuuawa kwa Mzee Ali Mohamed Kibao, Jasusi aliwatahadharisha Chadema kwamba kuna mpango wa viongozi waandamizi wa chama hicho kubambikiziwa kesi mauaji dhidi ya kiongozi huyo mwandamizi aliyeuawa kinyama na maiti yake kuharibiwa na tindikali.
Siku moja baadaye, msema ovyo maarufu Cyprian Musiba aliibuka na kuashiria kitu hichohicho alichotahadharisha Jasusi ambapo alilitaka jeshi la polisi kumhoji Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika.
Na jana jeshi la polisi limetangaza kuwa linamhitaji Mnyika kwa ajili ya mahojiano.
Na jana, Jasusi alitahadharisha kuhusu mpango wa kuwakamata viongozi wa Chadema, na in less than 2 hours, kada maarufu wa chama hicho, Boniface Jacob a.k.a Boni Yai alikamatwa.
Na kinachokera zaidi kuhusu Chadema, pindi makada wao wanapotukana watu wasio na hatia, viongozi wa chama hicho huwa hawakemei as if wanafurahia udhalilishaji unaofanywa na makada wao.
Mfano hai ni huu hapa
Hii twiti ya Martin ilimkwaza sana Jasusi na licha ya ku-reach out kwa Martin na kumpatia ufafanuzi wa alichokiita uongo wa Jasusi, hadi leo hajaifuta. Twiti hii ina views zaidi ya LAKI MBILI.
Hata hivyo, pamoja za dhihaka za akina Martin na kukosa ushirikiano kutoka kwa viongozi wa Chadema, Jasusi ameshawishika kuwapatia BURE ushauri huu wa kiintelijensia ambao hawawezi kuupata mahala popote pale.
TANGAZO
Utangulizi
Mpango huu wa kimkakati unalenga kuwasaidia Chadema kuhakikisha maandamano yao yanafanikiwa licha ya juhudi zozote za kuyazuia. Ni muhimu kuzingatia kwamba ushauri wote unapaswa kutekelezwa kwa njia za amani na kisheria.