Urais Zanzibar: Kwa Kurejea Hujuma Dhidi Yake 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, Maalim Seif Ana Haki Kugombea Tena Kwa Mara ya Sita

Jana, mwenyekiti wa taifa wa ACT-Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad alitangza kuwa ataomba ridhaa ya chama chake kuwa mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho.


Endapo atapitishwa, na kwa mtazamo wangu sioni cha kuzuwia yeye kupitishwa na chama hicho, itakuwa ni uchaguzi mkuu wa tano mfululizo kwa Maalim Seif kugombea nafasi hiyo. Historia ya kugombea kwake urais wa Zanzibar ni kama ifuatavyo:
Aligombea mwaka 1995 katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi dhidi ya mgombea wa CCM Dkt Salmin Amour, alieshinda kwa asilimia 50.2 ilhali Maalim Seif alipata asilimia 49.8
Akagombea tena mwaka 2000 akichuana na mgombea wa CCM Amani Karume aliyeshinda kwa asilimia 67.04 huku Maalim Seif akipata asilimia 32.96
Alijaribu tena bahati yake mwaka 2005 dhidi ya mgombea wa CCM Amani Karume aliyeshinda kwa asilimia 53.2 huku Maalim Seif akifuatia kwa karibu kwa asilimia 46.1
Katika uchaguzi wa mwaka 2010 Maalim Seif alianguka tena akipata asilimia 49.14 huku mgombea wa CCM Ali Mohammed Shein ashinda kwa asilimia 50.11
Na uchaguzi mkuu wa mwisho kabla ya huu wa mwaka huu ulifanyika mwaka 2015 ambapo katika kinachoweza kutafsiriwa kuwa hujuma za waziwazi dhidi ya Maalim Seif, Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar ilifuta matokeo ya uchaguzi, na kuamuru urudiwe ambapo Maalim Seif alisusa, na Dkt Shein akatangazwa mshindi kwa asilimia 91.4 matokeo ambayo hadi leo Maalim Seif hayatambui.

Hata hivyo, uamuzi wa Maalim Seif kutangaza kuwania tena urais kwa mara ya sita mfululizo kumezua maswali ambapo baadhi ya watu wanadhani ingekuwa mwafaka apishe wanasiasa wengine kuwania nafasi hiyo, hasa kwa vile amekuwa akishindwa chaguzi zote alizoshiriki.

Mwanaharakati Mzalendo @MwanaharakatiMz
Mwenyekiti wa Chama Cha @ACTwazalendo Maalim Seif Sharif Hamad ametangaza nia ya kuomba ridhaa ya chama chake kugombea Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu 2020. Hii itakuwa mara ya 6 kwa Maalim kugombea nafasi hiyo. https://t.co/hmi645WjZsKwa mtazamo wangu -unaoweza kuwa sio sahihi - sidhani kama kuna tatizo kwa Maalim Seif kugombea tena ENDAPO wafuasi wa chama chake wanaamini ndio mtu sahihi kuwa mgombea wao. Ikumbukwe kuwa hakuna ushahidi wowote kuwa Maalim Seif au ACT-Wazalendo wamemzuwia mwanachama mwingine kujitokeza kuwania nafasi hiyo. Na huenda akajitokeza leo au kabla ya zoezi la kutangaza nia kufungwa.
Lakini jingine ni haki ya kikatiba kwa Maalim Seif kugombea nafasi hiyo na nyingineyo ambayo ana sifa stahili.
Kadhalika, yeye ni mzoefu wa siasa za Zanzibar pengine zaidi ya mwanasiasa mwingine yoyote yule na amekumbana na misukosuko mingi katika kupigania haki, hususan za Wapemba.
Pengine kubwa zaidi ni “siri ya wazi” kuwa Maalim Seif amekuwa akiporwa ushindi mfululizo. Kwahiyo wanaomlaumu kwa “kugombea kila uchaguzi” wanapaswa pia kufahamu kuwa “aliporwa haki yake katika kila chaguzi hizo.” Sasa kwa vile kukata tamaa dhidi ya wanaomhujumu hakutobadili chochote basi ni vema akajaribu tena mwaka huu.
Hata hivyo, kuwa mgombea ni kitu kimoja na kushinda kwenye uchaguzi ni kitu kingine kabisa. Na hakuna mtu anayelielewa hilo vema zaidi ya Maalim Seif kwani licha ya maandalizi ya kila hali, ameishia kushindwa kila uchaguzi si kwa vile “kura hzikutosha” bali “sanaa za kiza” zimekuwa zikutumika kupora ushindi wake. Naandika hili kwa sababu nilipokuwa Kitengo nilishuhudia kwa macho yangu hujuma zilizofanywa dhidi ya mwanasiasa huyo, na ndio maana nadhani ni sahihi kwake kujaribu tena “kudai haki yake.”
Nimeandika hapo awali kwamba kuwa mgombea ni jambo moja na kushinda ni jingine. Swali linalobaki ni kwamba endapo atapitishwa na chama chake, na hilo sina shaka nalo, je atafanikiwa kuwa Rais ajaye wa Zanzibar?
Naomba nihifadhi jibu hadi CCM itakapopitisha mgombea wake ambapo kwa jicho la kijasusi nadhani atakuwa kati ya Dkt Mwinyi na Prof Mbarawa (naomba usininyime pongezi zangu kwa ‘ubashiri wangu’ endapo mmoja wao atapitishwa😊 )
Lakini wakati mnasubiri jawabu langu kwa swali endapo Maalim Seif atashinda, niwafikirishe tu na kauli mbili zinazokinzana kutoka kwa mwanasiasa huyo.


Kisha


Maana yake ni kwamba Maalim Seif anaamini kuwa yeye na chama chake wanaweza kushinda hata kama kasoro alizoongelea kwenye makala hiyo (ya gazeti la Daily Maverick la Afrika Kusini) hazitorekebishwa.
Nisingependa kuongelea sana hilo kwa sasa maana mada hii imejikita kwenye tangazo la Maalim Seif kuwania tena nafasi ya urais na sio uchambuzi wa kina kuhusu mwanasiasa huyo na/au uchaguzi wa Zanzibar kwa ujumla, ambao utakujia mara baada ya Maalim Seif kupitishwa rasmi na CCM kutangaza mgombea wake.
Nimalizie kwa tangazo kuhusu vitabu vyangu vinavyopatikana HAPA. Endapo utakumbana na usumbufu wowote, nishtue.

Ndimi jasusi wako.
Evarist Chahali
Create your profile
Only paid subscribers can comment on this post
Check your email
For your security, we need to re-authenticate you.
Click the link we sent to , or click here to sign in.