Urais Kwa Tiketi Ya Chadema: 'Mgombea Kutoka CCM' Yupo Kimkakati?

Moja wa watia nia ya kugombea urais kwa tiketi ya Chadema ni Mayrose Majinge, ambaye huko nyuma alikuwa mwana-CCM, na aliwahi kujaribu kuwania uenyekiti wa UWT Taifa bila mafanikio.

fedes kinunda (@connect_dots255) | Twitter

Pengine tatizo la jasusi wako ni kupenda “kuangalia kila tukio kwa jicho la kijasusi,” lakini tangu mwanamama huyu alipotangaza nia ya kutaka kuwania urais kwa tiketi ya Chadema, “hisia ya sita” ilitonya kuwa “huenda kuna namna.”

Live from EA Radio Super Breakfast: Mtangaza Nia Urais wa JMT ...

Si kwamba hana haki kugombea nafasi hiyo. Hapana. Alijiunga kihalali na Cahdema, na hajaficha kuwa aliwahi kuwa mwana-CCM. In fact, sidhani kama kuna mwanasiasa wa upinzani ambaye hajawahi kuwa mwana-CCM huko nyuma.

Kwanini “hisia ya sita ya jasusi wako” imeonyesha tahadhari? Kwa sababu kadhaa, miongoni mwao ikiwa uwezekano mkubwa wa CCM kujaribu kila mbinu kuhujumu Upinzani katika uchaguzi mkuu ujao, hususan Chadema na ACT-Wazalendo.

Mkakati wa Rais Magufuli sio tu kuhakikisha anarudi Ikulu kwa kishindo, bali pia anaangamiza “vyama halisi vya upinzani” ambavyo huhitaji kuwa mjuzi wa siasa za Tanzania kubaini kuwa ni Chadema na ACT-Wazalendo.

Na huhitaji kuwa jasusi mstaafu kama mie kubaini kuwa mwanamama huyo hatopitishwa na Chadema kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho. Rejea chapisho HILI kufahamu ubashiri wangu kuwa nani atapitishwa katika nafasi hiyo.

Kwahiyo, hisia ya sita inaniambia kuwa baada ya mwanamama huyo kukatwa jina lake, “ATALIANZISHA.” Aidha kwa kudai amebaguliwa kama mwanamke, au kwa kutumia “shaka iliyopo muda huu dhidi yake” kuwa “huenda katumwa na CCM” au kuzusha chochote kile. Nafsi inakataa kuamini kuwa atapokea kushindwa kwake kwa mikono miwili.

Lakini kama navyotanabaisha kila mara, ujasusi sio exact science. Mengi yanaweza kutokea kati ya leo na hapo Chadema watakapotangaza mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama hicho. Kwahiyo “nisikaliwe kooni” endapo hali haitokuwa hivyo - na sie wapenda demokrasia tunaomba zoezi hilo liishe kwa amani.

Nimalizie kwa kukusihi ukae mkao wa kula

Ndimi jasusi wako

Evarist Chahali