Ujumbe Maridhawa Kutoka Kwa Mtumishi wa Mungu Dkt Bagonza

Mtumishi wa Mungu Dkt Bagonza a naendelea kuwa moja ya sauti adimu kabisa katika zama hizi za utawala wa kidikteta wa Jiwe aka “Dkt Evil.”

Tatizo ambalo Dkt Bagonza anajibidiisha kulishughulikia ni ukweli kwamba (a) kukaa kimya hakuwezi kumfanya Dkt Evil apatwe na huruma (b) actually ukimya wa wahanga wa udikteta unaweza kumpa moyo dikteta husika kuwa wanaafikiana nae (c) kukalia kimya jambo baya kunachangia ustawi wa jambo hilo.

Unaweza kuungana na Dkt Bagonza kwa kufanya sala/dua binafsi kwa Mola wako kuomba alete mwisho wa udhalimu unaoendelea.

Nimalizie kwa matangazo mawili. Kwanza nina furaha kuchapisha vitabu vitano vya bure. Vitabu hivi ni mkusanyiko wa twiti za kumhamasisha mtu katika mazingira mbalimbali sambamba na kusaidia kumfanya awe mtu bora/kuboresha ubora wake, kwa kimombo tunaita “motivational tweets.”

Vitabu hivi vitakuwa vinachapishwa kila mwezi na vitaendelea kutolewa bure. Baadaye nitatangaza utaratibu wa kuvipata (baada ya ule wa awali kuwataka watu wajisajili kutokuwa na ufanisi).

Tangazo jingine ni kuhusu ofa hii ya kuanzia mwaka 2020

Ndimi mtumishi wako wako,

Evarist Chahali