Barua Ya Chahali

Barua Ya Chahali

Share this post

Barua Ya Chahali
Barua Ya Chahali
UJASUSI (espionage) ni nini? Na MAJASUSI (spies) wanafanya kazi gani hasa? [Sehemu ya Kumi na Tatu: kufuatiliwa (surveillance) na jinsi jasusi anavyowakwepa wanaomfuatilia]
Copy link
Facebook
Email
Notes
More
Simulizi za Jasusi

UJASUSI (espionage) ni nini? Na MAJASUSI (spies) wanafanya kazi gani hasa? [Sehemu ya Kumi na Tatu: kufuatiliwa (surveillance) na jinsi jasusi anavyowakwepa wanaomfuatilia]

Evarist Chahali's avatar
Evarist Chahali
Jun 11, 2023
∙ Paid
1

Share this post

Barua Ya Chahali
Barua Ya Chahali
UJASUSI (espionage) ni nini? Na MAJASUSI (spies) wanafanya kazi gani hasa? [Sehemu ya Kumi na Tatu: kufuatiliwa (surveillance) na jinsi jasusi anavyowakwepa wanaomfuatilia]
Copy link
Facebook
Email
Notes
More
Share

Hii ni makala ya kumi na tatu katika mlolongo mrefu wa makala mbalimbali zinazohusu taaluma ya intelijensia. Huenda baadhi ya makala hizi zikazaa vitabu huko mbeleni kama ambavyo makala kuhusu “Afisa Usalama wa Taifa ni Mtu Gani? Na Anafanya Nini?” zilivyopelekea kitabu bora kabisa chenye jina hilo.

Afisa Usalama wa Taifa ni Mtu wa Aina Gani na Anafanya Nini, shushushu

Makala/Sehemu ya kwanza ilihusu maana ya neno UJASUSI. Ni vema ukasoma sehemu ya kwanza na ya pili kabla ya kusoma sehemu ya tatu.

Soma makala ya kwanza hapa

Makala ya pili ilihusu historia ya ujasusi

Soma makala ya pili hapa

Makala ya tatu ilihusu aina za ujasusi

Soma makala ya tatu hapa

Makala ya nne ilimalizia kilichosalia katika sehemu ya tatu kuhusu aina za ujasusi.

Soma makala ya nne hapa

Makala ya tano ilihusu ujasusi kama nyenzo ya kidiplomasia

Soma makala ya tano hapa

Makala ya sita ilihusu ujasusi wa kidiplomasia

Soma makala ya sita hapa

Makala ya saba ilihusu kifuniko (cover) cha jasusi

Soma makala ya saba hapa

Makala ya nane ilihusu tofauti kati ya ujasusi na uafisa usalama wa taifa

Soma makala ya nane hapa

Makala ya tisa ilihusu jinsi majasusi wanavyopatikana

Soma makala ya tisa hapa

Makala ya kumi ilihusu jinsi jasusi anavyopata watoa habari nje ya nchi na kujipenyeza eneo kusudiwa.

Soma makala ya kumi hapa

Makala ya kumi na moja ilieleza kuhusu majasusi wakiwa kazini

Soma makala ya kumi na moja hapa

Makala ya kumi na mbili ilihitimisha kuhusu majasusi wanavyokuwa kazini huku wakiwa na “roho mkononi”

Soma makala ya kumi na mbili hapa

Hata hivyo, kabla ya kuingia kwa undani, ni vema kujikumbusha kuwa mpangilio wa mada zinazounda mfululizo wa makala hizi, ambao ni kama ifuatavyo:

👉Maana ya ujasusi

👉 Historia ya Ujasusi

👉 Aina za Ujasusi

👉 Ujasusi wa kimtandao

👉Ujasusi kama nyenzo ya diplomasia

👉Ujasusi wa kidiplomasia

👉Kifuniko (cover) cha Jasusi

👉 Tofauti kati ya Ujasusi na Uafisa Usalama wa Taifa

👉 Majasusi wanapatikanaje?

👉Jinsi jasusi anavyopata watoa habari nje ya nchi na kujipenyeza eneo kusudiwa.

👉 Majasusi kazini

👉 Changamoto zinazoukabili ujasusi/majasusi duniani

👉 Changamoto za ujasusi/majasusi Tanzania

👉 Mashirika maarufu ya ujasusi duniani na majasusi maarufu duniani.

Makala hii inayojitegemea japo inahusiana na “majasusi kazini” inaelezea kuhusu hatari inayomkabili kila jasusi anapokuwa nje ya nchi, yaani KUFUATILIWA au kwa Kiingereza “surveillance”.

Hadi kufikia hapa utakuwa umeshapata picha kuwa ujasusi ni kama mchezo wa kuwindana, na kufanikiwa au kufeli hutegemea “anayemzidi akili/maarifa mwenzie.”

Utakumbuka pia iliongelewa katika makala iliyopita kuhusu mwamko kuhusu adui (adversarial awareness), na ukatajiwa maeneo makuu matatu.

Mwamko kuhusu adui unatilia mkazo maeneo makuu matatu

👉Kupuuza (ignorance): hapa adui hana taarifa ya uwepo wa jasusi wa kigeni. Katika ujasusi, kila jitihada inafanyika kuhakikisha kuwa adui anabaki kwenye hatua hii.

👉Kuchunguza (probing): hapa adui anahisi kuhusu uwepo wa jasusi na/au shughuli za kijasusi, na ikithibitika anahamia hatua ya kulenga (targeting). Lakini akijiridhisha kuwa hakuna lolote, anarudi katika hatu ya kupuuza (ignorance).

👉Kulenga (targeting): hapa adui ameshajiridhisha kuhusu uwepo wa jasusi na sasa anafuatilia nyendo zake.

Kwahiyo, ili jasusi aweze kuifanya Idara ya Usalama wa Taifa wa nchi husika isimshtukie, yaani hapo kwenye eneo la kupuuza (ignorance) kama ilivyotanabaisha hapo juu, ni LAZIMA amudu kuepuka kufuatiliwa.

This post is for subscribers in the Founding Member plan

Already in the Founding Member plan? Sign in
© 2025 Evarist Chahali
Privacy ∙ Terms ∙ Collection notice
Start writingGet the app
Substack is the home for great culture

Share

Copy link
Facebook
Email
Notes
More