Uchunguzi wa Kiintelijensia: Je Deusdedit Soka na Wenzake "Waliotekwa" Wapo Hai Au La?
Wiki chache zilizopita, mwanaharakati mmoja wa Chadema alimtumia ujumbe (DM) Jasusi akiuliza kama ana taarifa zozote kuhusu “(Deusdedit) Soka na wenzake”.
Jasusi hajajibu ujumbe huo hadi leo. Kwa sababu kadhaa.
TANGAZO
Ya kwanza ni kutoharibu uchunguzi ambao Jasusi amekuwa akiufanya binafsi kuhusiana na suala hilo. Kwanini Jasusi afanye ucuhunguzi binafsi? Kwa sababu kadhaa lakini moja ni utumishi kwa umma, na mara kadhaa Jasusi amejitambulisha kama “Mtumishi Wako/Wenu”.
Kwa sababu ukiaminiwa na watu, aminika. Na ili uaminike, shurti uwapatie sababu ya msingi hao wanaokuamini. Na moja ya sababu ya Jasusi kuaminika ni kutokurupuka na taarifa kwa ajili tu ya kupata likes, views, RTs, nk, jambo ambalo limeshamiri mno kwenye mitandao ya kijamii.