Uchambuzi wa kijasusi: uteuzi wa Mkuu wa Majeshi na Mnadhimu Mkuu mpya - kwanini Luteni Jenerali Mkingule 'amerukwa' na kuishia kupewa ubalozi?
Jana, Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi, akichukua nafasi ya Jenerali Venance Mabayo anayestaafu. Sambamba na uteuzi huo, Rais pia amempandisha cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni Jenerali kisha akamteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ.
Kwa wenye kumbukumbu nzuri, mtakumbuka kuwa Mei 24 mwaka jana, Jasusi alibashiri kitu kuhusu Luteni Jenerali Othman
Makofi kwa jasusi tafadhali 😊
Enewei, lengo la makala hii ya kijasusi ni kuchambua kwanini mtu aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kuwa Mkuu wa Majeshi, ambaye hadi jana alikuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Mathew Mkingule sio tu “amerukwa” bali pia “ameshushwa cheo kidiplomasia” na kupewa ubalozi.






