[Reposted] Uchambuzi wa kiintelijensia: tathmini ya mwaka mmoja wa urais wa Mama @SuluhuSamia, na mustakabali wa uongozi wake kuelekea 2025
Leo, Machi 19, ni mwaka mmoja kamili tangu Mama Samia Suluhu Hassan aaipishwe kuwa Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mara baada ya kuapishwa, jasusi wako niliahidi kukuletea “ubashiri” (kijasusi wanaita “predictory intelligence”) kuhusu mustakabali wa urais wa kiongozi huyo.
Ikumbukwe kuwa miezi 20 iliyopita, Mei 19, 2021, jasusi Evarist Chahali alichapisha “ubashiri” kuhusu mustakabali wa urais wa Rais Magufuli kwa jinsi alivyokuwa anashughulikia (or rather kupuuzia) janga la korona, na akatanabaisha kuwa janga hilo lingegharimu urais na uhai wake.


Na ikawa hivyo Machi 12 mwaka jana

japo serikali ilitangaza rasmi siku tano baadaye

Uchambuzi huu wa kiintelijensia uliofanyika kwa kutumia mbinu mbalimbali za uchambuzi wa kiintelijensia, na ambao umegharimu mwaka mzima kuukamilisha, unaanza kwa tathmini ya “jinsi gani hasa Mama Samia aliingia madarakani,” ikiwa ni pamoja na kugusia madai kuwa “aliandaliwa kimkakati mwaka 2015 aje kuwa Rais badala ya Magufuli.”
Kadhalika, uchambuzi utaangalia kwa kifupi urais wake katika kipindi cha mwaka mzima, tangu aapishwe kuwa Rais Machi 19 mwaka jana.
Katika hitimisho, uchambuzi huu wa kiintelijensia utabashiri kwa uyakinifu kama
👉 atafika mwaka 2025 (ambapo kuna na uchaguzi mkuu mwingine)?
na “akifika hiyo 2025
👉je atagombea urais?”
na akigombea urais hiyo 2025, endapo akifika,
👉je atashinda?”