Uchambuzi wa Kiintelijensia: Ndugai Kumkosoa Mama Samia Waziwazi Kuhusu Mikopo na Utetezi wa Mama Samia Jana, Na Kauli ya Nabii Mwingira Kuhusu Alivyonusurika Mara 3 Kuuawa Enzi za JPM
Matukio yanayotawala anga za habari za Tanzania, na yanayoweza kabisa kuitwa “funga mwaka,” ni matatu. La kwanza ni tamko la majuzi la kiongozi maarufu wa dini, Nabii Josephat Mwingira, ambaye katika mahubiri yake alielezea masahibu yaliyomkumba wakati wa utawala wa marehemu Magufuli.
Kufuatia tamko hilo zito lililotanabaisha kuwa kulikuwa na majaribio matatu ya kumtoa uhai, sambamba na kuuawa kwa binti aliyemfahamisha kiongozi huyo wa dini kuwa kuna mpango wa kumdhuru, Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene aliagiza Nabii Mwingira ahojiwe, kabla ya jeshi la polisi kumtaka ajisalimishe kwa mahojiano.
Kabla vumbi halijatulia, kukapatikana video ya hotuba ya Spika wa Bunge la Muungano, Job Ndugai, akimkosoa waziwazi Mama Samia Suluhu kuhusu serikali yake kuendelea kukopa huku Tanzania ikiwa inakabiliwa na deni la shilingi trilioni 70. Ndugai alikwenda mbali na kudai ipo siku Tanzania inaweza kupigwa mnada kutokana na madeni.
Siku moja baadaye, jana, Mama Samia alimjibu Spika Ndugai, ambapo pamoja na mambo mengine alieleza kuwa mikopo inayokopwa ni ya lazima kutokana na uwepo wa miradi aliyoikuta yeye alipoingia madarakani ambayo anawajibika kuiendeleza.
Uchambuzi huu wa kiintelijensia unatoa tafsiri pana ya matukio hayo matatu, sambamba na impacts zake katika mwaka mpya 2022 na beyond.