Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu mkutano wa majadiliano kati ya Mama @SuluhuSamia na viongozi wakuu wa Chadema
Rais Samia Suluhu Hassan jana alikutana na viongozi wakuu wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Mheshimiwa Freeman Mbowe, katika mkutano wa majadiliano ulifanyika Ikulu ya Chamwino huko Dodoma.
Kama ilivyokuwa kwenye matukio mawili ya Rais Samia kukutana na Mheshimiwa Mbowe, Machi 4 mwaka huu na majuzi Mei 9, taarifa za mkutano wa jana hazikufahamika hadi baada ya mkutano huo kukamilika.
Kwa upande wa Mheshimiwa Mbowe, mkutano wa jana ni watatu kwa yeye kukutana na Rais Samia, ambapo kama ilivyoelezwa hapo juu, viongozi hao wawili walikutana Machi 4 mwaka huu siku ambayo Mheshimiwa Mbowe alitoka jela kufuatia kufutwa kwa kesi ya ugaidi na uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili
Kisha viongozi hao walikutana tena majuzi Mei 9
Hata hivyo, tofauti na mikutano hiyo miwili, mkutano wa jana uliwahusisha viongozi wengine waandamizi wa Chadema na CCM.
Uchambuzi huu wa kiintelijensia unajikita katika kukuwezesha “kusikia ambayo hayajatamkwa” na “kuona ambayo hayajaonyeshwa.”