Uchambuzi wa Kiintelijensia Kuhusu Mkutano Baina ya Mama Samia na Tundu Lissu Nchini Ubelgiji Hapo Jana
Jana, Februari 16 ya mwaka huu 2022, itaingia kwenye kumbukumbu za historia ya Tanzania baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kukutana na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, mjini Brussels, Ubelgiji, ambako Mama Samia yupo kwenye ziara ya kikazi.
Tetesi kwamba Mama Samia angekutana na Lissu zilianza kusikika asubuhi ya jana, na kufikia mchana kulikuwa na kila dalili za kutokea tukio hilo muhimu.
Itakuwa habari njema endapo Lissu atakutana na Mama @SuluhuSamia huko Ubelgiji. Habari njema kwa kila anayeitakia mema Tanzania yetu. Hata hivyo, itakuwa habari mbaya mno kwa "wanaonufaika na mifarakano ya kisiasa," na sintoshangaa kusikia "wanaharakati" wakimuwashia moto Lissu
Na muda mfupi baadaye, ikatolewa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo muhimu
Makala hii ya kiintelijensia inaeleza mazingira yaliyopelekea kufanyika kwa mkutano huo, na kubwa zaidi, mustakabali wa siasa za Tanzania kwa upande mmoja, maisha ya kisiasa ya Lissu, na kwa mbali kidogo, hatma ya kesi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.