Barua Ya Chahali

Share this post
Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu Jenerali Mabeyo: anastaafu au 'ameondolewa kidiplomasia'? Nani kumrithi? 'Mazuri' na 'mabaya' yake
www.baruayachahali.com

Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu Jenerali Mabeyo: anastaafu au 'ameondolewa kidiplomasia'? Nani kumrithi? 'Mazuri' na 'mabaya' yake

Evarist Chahali
Jun 6
9
Share this post
Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu Jenerali Mabeyo: anastaafu au 'ameondolewa kidiplomasia'? Nani kumrithi? 'Mazuri' na 'mabaya' yake
www.baruayachahali.com
Read Barua Ya Chahali in the new Substack app
Now available for iOS

Nini kimetokea? Leo Jumatatu Juni 6, 2022 imetangazwa kuwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo anastaafu mwishoni mwa mwezi huu.

Jenerali Mabeyo ni nani hasa? Jenerali Venance Mabeyo ni Mkuu wa Majeshi wa nane kuliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tangu alipoteuliwa Februari 6, 2017 na aliyekuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Mabeyo baada ya kulitumia Jeshi kwa nafasi mbalimbali kuanzia 1 Januari 1979, mwishoni mwa mwezi huu atastaafu utumishi ndani ya jeshi hilo.

Alizaliwa Julai 1, 1956 wilayani Magu mkoani Mwanza na kupata elimu ya msingi katika shule ya Namibu mkoani Mara kuanzia 1965 hadi 1971.

Alianza elimu ya Sekondari katika Seminari ya Nyegezi kuanzia 1972 hadi 1975, kisha akaendelea na kidato cha tano na sita Mzumbe Sekondari kuanzia 1976 hadi 1977.

Jenerali Venance Mabeyo alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Januari 1, 1979 na kuhudhuria kozi ya afisa mwanafunzi na kupata kamisheni mwaka 1980 kuwa Luteni Usu.

Safari ya Jenerali Venance Mabeyo JWTZ Julai 1980: Luteni Usu Agosti 1981: Luteni Januari 1987: Kapteni Oktoba 1991: Meja Juni 1998: Luteni Kanali Mei 2006: Kanali Septemba 2010: Brigedia Jenerali Septemba 2014: Meja Jenerali Juni 2016: Luteni Jenerali Februari 2017: Jenerali

Jenerali Venance Mabeyo alihudhuria kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi, baadhi ya nchi hizo ni Kenya, India, Canada na Marekani.

Jenerali Venance Mabeyo katika kulitumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania alishika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mwambata Jeshi nchini Rwanda, Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Tawi la Usalama na Utambuzi na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ.

Jenerali Venance Mabeyo ametunukiwa medali mbalimbali; Miaka 20 ya JWTZ Medali ya utumishi mrefu. Medali ya miaka 40 ya JWTZ. Medali ya utumishi uliotukuka. Medali ya Comoro na Anjouan. Medali ya miaka 50 ya uhuru Medali ya miaka 50 ya Muungano Miaka 50 ya JWTZ Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Anastaafu kweli au ameondolewa kidiplomasia? Anastaafu kwa hiari yake. Tangu Rais Samia Suluhu alipoingia madarakani, ilifahamika kuwa Jenerali Mabeyo alikuwa mbioni kustaafu lakini akalazimika kubaki madarakani kumsaidia Rais Samia katika kipindi cha mpito.

Nani anatarajiwa kumrithi?

Twitter avatar for @Chahali𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 @Chahali
Curious Cat: Jasusi, je nani atamrithi Jenerali Mabeyo anayestaafu mwezi huu? Jasusi: Dear Cat, unanipa jukumu la kuwa "Sheikh Yahya" (unajimu) ilhali mie ni jasusi. Hata hivyo, naweza kuhisi Luteni Jenerali Matthew Mkingule. Keyword hapo ni "kuhisi" 😊

𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 @Chahali

Nimefahamishwa kuwa Mama @SuluhuSamia amempandisha cheo Meja Jenerali Matthew Mkingule kuwa Luteni Jenerali na kumteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ. Hata hivyo taarifa hizi hazijathibitishwa. Nitawajulisha zaidi https://t.co/KYDfpyrGiW

June 6th 2022

1 Retweet8 Likes

Hata hivyo, HISIA kwamba mrithi wa Jenerali Mabeyo ni Luteni Jenerali Mkingule hazimaanishi kuwa LAZIMA itakuwa hivyo. Japo kwa sasa Tanzania ina Luteni Jenerali mmoja tu, ambacho ni cheo cha pili nyuma ya Jenerali, Rais ana uwezo wa kumpandisha cheo mmoja wa ma-Meja Jenerali kadhaa walio chini ya Luteni Jenerali Mkingule, na kumpa mteuliwa Ukuu wa Majeshi, japo haitarajiwi kuwa hivyo.

Jenerali Mabeyo atakumbukwa kwa “mazuri” gani?

Kwa jasusi, kubwa zaidi ya yote ni jinsi yeye alivyokuwa sehemu ya “utatu mtakatifu” uliofanya jitihada kubwa kuhakikisha kuwa Katiba inaheshimiwa, baada ya kifo cha Rais John Magufuli, ambapo kulikuwa na jitihada za “kumruka” Mama Samia, aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo, na ambaye Kikatiba ndiye alipaswa kuapishwa kuwa Rais.

“Utatu mtakatifu” huo uliundwa na maafande wawili - Jenerali Mabeyo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Sirro - na mwanasiasa mmoja, Mheshimiwa Zitto Kabwe.

Ikumbukwe kuwa kama ilivyo kwa IGP Sirro, Jenerali Mabeyo pia alikuwa mtu wa Kanda ya Ziwa, na katika mazingira ya wakati huo ambapo kulikuwa na upinzani mkali dhidi ya Mama Samia, ingetarajiwa maafande hao nao waungane na “wapinzani wa Mama Samia,” lakini badala yake wakaweka nguvu zao kwenye kuhakikisha Katiba inaheshimiwa. Na ikiwa hivyo.

Yayumkinika kutanabaisha kuwa laiti maafande hao wangeungana na na “wana-Kanda ya Ziwa wenzao” waliotaka Katiba ipindishwe, Mama Samia “arukwe” na badala yake achaguliwe “mtu wao,” sijui hali ingekuwaje muda huu.

Jenerali Mabeyo atakumbukwa kwa “mabaya” gani?

Pengine si kwa makusudi, lakini Jenerali Mabeyo alikuwa mmoja wa “enablers” wa Magufuli, yaani watu waliowezesha maovu yaliyojiri kwenye utawala huo kufanyika.

Katika hilo, Jenerali Mabeyo, ni juu ya nafsi/nadhiri yake kumsuta. Yaliyojiri kwenye operesheni ya MKIRU na nyinginezo alizoagizwa na Magufuli “hayaandikiki” lakini yatarajiwa kuwa katika kustaafu kwake, afande huyo atapata fursa ya kutafakuri, na pengine “kutubu kwa Muumba wake.”

Utetezi kwake ni “je angeweza kuwa na ujasiri wa kupingana na matakwa ya Amiri Jeshi mkuu wake?” Ikumbukwe kuwa jeshini hakuna fursa ya kuhoji amri bali kutekeleza tu.

Kustaafu kwake kunaashiria ujio wa kustaafu wakuu wengine wa vyombo vya dola?

Exactly.

Twitter avatar for @Chahali𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 @Chahali
Next... IGP Sirro. And DGIS Diwani. In no particular order. Otherwise, it's high time Mama @SuluhuSamia has her own "siloviki".
Image

June 6th 2022

2 Retweets29 Likes

Hitimisho:

Barua ya Chahali itakuletea taarifa zaidi za mabadiliko tarajiwa huko Jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa.

Fanya kuunga mkono kijarida hiki kwa kuwa “kuchangia kama mwanachama” (paid subscriber).

Share this post
Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu Jenerali Mabeyo: anastaafu au 'ameondolewa kidiplomasia'? Nani kumrithi? 'Mazuri' na 'mabaya' yake
www.baruayachahali.com
TopNewCommunity

No posts

Ready for more?

© 2022 Evarist Chahali
Privacy ∙ Terms ∙ Collection notice
Publish on Substack Get the app
Substack is the home for great writing