Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu kujiuzulu kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Kanali Abdulrahman Kinana
Tanzania jana ilikumbwa na mshtuko mkubwa kufatia kujiuzulu kwa Makamu wa Mwenyekiti wa CCM, Kanali Abdulrahman Kinana.
Kujiuzulu kwa Kinana kumekuja siku chache tu baada ya makada maarufu wa chama hicho tawala, January Makamba na Nape Nnauye kuondolewa katika baraza la mawaziri la Rais Samia Sulumu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Uchambuzi huu wa kiintelijensia unabainisha sababu zilizopelekea Kinana kujiuzulu, sambamba na kueleza athari za kujiuzulu huko.