Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu taarifa zilizozagaa kuwa bandari ya Dar "imekodishwa kwa Waarabu kwa miaka 100".
Nini? Taarifa kwamba serikali ya Tanzania imeingia mkataba na “waarabu” na kwamba bandari ya Dar imekodishwa kwa waarabu hao kwa miaka 100.
Wapi? Taarifa zimesambaa zaidi kwenye mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kwenye “magrupu” ya Watanzania ya Whatsapp na Facebook.
Lakini pia kuna taarifa rasmi za Bunge la Muungano kukaribisha maoni kuhusu “mkataba huo wa miaka 100” (japo hakuna idadi ya miaka kwenye taarifa hii ya bunge)
Nani? Angalau nyaraka moja miongoni mwa kadhaa zilizosambaa inaonyesha Rais Samia Suluhu akimruhusu Waziri wa Ujenzi Profesa Mbarawa kutia saini mkataba husika
Kadhalika, mtawala wa Dubai Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum ametajwa kuwa ndiye mmiliki wa kampuni ya DP World inayodaiwa itakuchukua uendeshaji wa bandari ya Dar
Vilevile kumezagaa picha za Rais Samia akiwa na “mwanafamilia ya kifalme ya Dubai”
Lini? Kuna tarehe kadhaa kuhusiana na taarifa hii. Februari 22 mwaka jana Tanzania, kupitia Mamlaka ya Bandari (TPA) ilisaini mkataba wa awali na kampuni ya DP World wenye thamani ya dola milioni 500. Shughuli hiyo ilishuhudiwa na Rais Samia.
Lakini pia kuna hiyo Oktoba 3 mwaka jana ambapo Rais Samia alimkabidhi madaraka Waziri wa Ujenzi Profesa Mbarawa kuingia mkataba na serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii na kuboresha utendaji wa bandari za bahari na maziwa nchini Tanzania.
Vipi? Taarifa hizo zimejikita zaidi katika dhana kuwa “nchi inauzwa”
Sambamba na kukumbushia “angalizo” la aliyekuwa Spika wa Bunge la Muungano Job Ndugai aliyelazimika kujiuzulu baada ya kusema “kuna siku nchi itapigwa mnada”.
Uchambuzi wa kiintelijensia