Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu uamuzi wa Rais Samia kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa, ni fursa au "kitanzi" kwa Wapinzani?
Jana, Rais Samia Suluhu alikutana na viongozi wakuu wa vyama vya siasa, Ikulu, kubwa lililojiri katika mkutano huo ni uamuzi wake wa kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa.
Ni muhimu kufahamu kuwa ruhusa ilipaswa kuitwa “ruhusa kwa vyama vya upinzani kufanya mikutano ya hadhara” kwa sababu katika muda wote, chama tawala CCM kimekuwa kikifanya mikutano yake bila tatizo.
Uchambuzi huu wa kiintelijensia unaangalia jinsi gani uamuzi huo unavyoweza kuwa na faida au hasara kwa vyama vya upinzani, sambamba na faida/hasara kwa CCM.
Kubwa zaidi, “maridhiano” hayo yatawanufaisha vipi wananchi wa kawaida hasa katika kipindi hiki cha mgao wa umeme na maji