Uchambuzi wa Kiintelijensia: Jinsi Dkt Tulia Alivyopenya Mchujo wa Kuwania Uspika. Je Baada ya Kupata Uspika (na Hilo Halina Mjadala), Atakuwa 'Asset' au 'Liability' Kwa Utawala wa Mama Samia?
Hatimaye kinyang’anyiro cha kumpata mgombea wa nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano, kupitia chama tawala CCM, kimefikia ukingoni kwa chama hicho kumpitisha Naibu Spika wa sasa, Dkt Tulia Ackson.
Wana-CCM 70 hivi walijitokeza kuwania nafasi hiyo, huku mwanasiasa mkongwe Andrew Chenge akipewa nafasi kubwa. Licha ya Chenge, mwanasiasa mwingine aliyedhaniwa kuwa na nafasi nzuri ni Stephen Masele. Kadhalika, Mbunge wa Ilala kwa tiketi ya CCM, Mussa Hassan Zungu, naye alikuwa akitajwa kama mmoja wa “frontrunners.”
Je Dkt Tulia amewezaje kupenya kinyang’anyiro hicho dhidi ya mkongwe Chenge? Wakati ni wazi kwamba hakuna wa kumzuwia Dkt Tulia kuwa Spika ajaye, swali kubwa ni endapo katika Uspika wake atakuwa “asset” au “liability” kwa utawala wa Mama Samia.
Lakini swali jingine la muhimu ni imekuwaje hadi Chenge kukosa nafasi hiyo muhimu licha ya nguvu zake kubwa kisiasa?