Uchambuzi mfupi wa kiintelijensia kuhusu hatua ya Wenje kutangaza nia ya kuwania nafasi anayoshikilia Lissu
Nini?
Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Victoria, Ezekia Wenje ametangaza nia ya kuwania nafasi ya makamu mwenyekiti wa chama hicho-Bara.
Taarifa zilizopatikana jana zilieleza kwamba Wenje anakusudia kujitosa kuomba ridhaa ya nafasi hiyo ambayo kwa sasa inashikiliwa na Tundu Lissu.
Alisema nini hasa?
Alitanabaisha dhamira hiyo jana alipozungumza na waandishi akisisitiza ameamua kuwania nafasi hiyo, ili kuongeza ufanisi wa kazi na uwajibikaji.
Wenje alidai kwamba baada ya tafakuri ya muda ameona ana uwezo wa kuwa msaidizi wa karibu wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye duru za kisiasa zinaonyesha atagombea tena uenyekiti kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
"Kutokana na uzoefu nilionao chamani, nimejitathimini kuwa nina uwezo wa kuwa msaidizi wa Mbowe, naomba ifahamike chama chetu cha Chadema kimekuwa kikijipambanua siku hadi siku katika kupigania haki za watu, ikiwemo uhuru, haki na maendeleo," amesema.
TANGAZO
Kwa walio nje ya Tanzania, vitabu vinapatikana HAPA
Lissu atagombea?
Hata hivyo, haijafahamika kama Lissu ambaye ni mbunge wa zamani wa Singida Mashariki atawania nafasi hiyo kwa mara nyingine au atapoumzika, kwani jitihada za kumtafuta kuzungumzia jambo hilo kwa njia ya simu zinaendelea, baada ya awali kutafutwa bila mafanikio.