#Uchaguzi2020: Membe Anaweza Kumwangusha Magufuli Endapo Atagombea Urais?

Jana, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Bernard Membe alikaririwa akisema kuwa anaweza kugombea urais endapo Wapinzani watampa ridhaa hiyo.

Binafsi sikupendezwa na kauli hiyo kwa sababu kuu moja. Wapinzani hawahitaji kumpa mtu ridhaa ya japo kuwa mwanachama wa chama husika, let alone ridhaa ya kuwa mgombea urais. Anayepaswa kuomba ridhaa iwe ya kuwa mwanachama, au kugombea uongozi - ikiwa ni pamoja na kugombea urais - ni Membe na si Wapinzani.

Hata hivyo, japo sikuafiki kauli yake, nimeelewa kwanini amesema hivyo. Ukweli mchungu kuhusu Wapinzani wetu ni mwendelezo wao wa kutegemea “watu kutoka CCM” kuwa wagombea wao kwenye uchaguzi mkuu.

Kama ilivyokuwa 2015 ambapo Wapinzani kupitia UKAWA walimteua Lowassa ambaye alibwagwa kwenye mchakato wa kuwania urais huko CCM, yayumkinika kuhisi kuwa hali hiyo yaweza kujirudia tena kwa Membe. Na ndio maana majuzi alikaribishwa na Zitto.

Hata hivyo japo kura hizi chache za maoni si sauti ya wengi, yawezekana kuna Watanzania mbalimbali - nami nikiwa mmoja wao - wanaokerwa kuona Wapinzani wakishindwa kuzalisha wagombea wenyewe na badala yake kutegemea “makapi” ya CCM.

Yayumkinika kuhisi kuwa kauli ya Membe jana ni kuitikia wito wa Zitto alioutoa juzi. Na yayumkinika kuhisi si ajabu Membe akitangaza kujiunga na ACT-Wazalendo na kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

Hilo si gumu, na kwa jinsi ACT-Wazalendo ilivyo, sitarajii kutokea upinzani wowote dhidi ya both ujio wa Membe na eventual decision ya kumfanya mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

Lililo gumu si tu Membe kufanikiwa kuwa Rais ajaye wa Tanzania, kwa maana ya kumng’oa madarakani Magufuli, bali pia kukiwezesha chama cha ACT-Wazalendo kutoka “chama kipya” cha upinzani hadi kuwa chama tawala.

Kwa wanaofuatilia makala zangu mbalimbali, nilishawahi kueleza kwa kina kwanini Membe hawezi kuwa rais. Moja ya makala hizo ni hii

Twitter avatar for @ChahaliEvarist Chahali @Chahali
Toleo la wiki hii la #BaruaYaChahali tayari limewasili kwenye inbox za subscribers. Jisajili
chahali.substack.com kijarida hiki bora kabisa kuliko vyote duniani kwa Kiswahili. Wiki hii: Membe na #Urais2020. Pia introducing paid subscription + 4 new newsletters from 01.07.19 Image

Pia waweza kusoma uchambuzi huu wa kina

Hata hivyo, kama walivyo majasusi wazoefu ambapo kila dakika inaweza kuwa tofauti na dakika iliyopita, yawezekana kabisa kuwa mtazamo wangu kuhusu Membe kwa wakati huu ni tofauti na huo uliomo kwenye makala hizo.

Simaanishi kuwa nimebadili mtazamo au nitabadili mtazamo bali natanabaisha tu kuwa HUENDA kukawa na tofauti. Kadhalika, ni muhimu kutambua kuwa mazingira ya wakati naandika makala/uchambuzi husika yanaweza kuwa tofauti na muda huu.

Naomba niishie hapa kwa kuahidi UCHAMBUZI WA KINA WA KIINTELIJENSIA endapo Membe atajiunga na ACT-Wazalendo, ambapo kwa jicho langu la kijasusi nahisi itakuwa hivyo kama nilivyobashiri awali

Ndimi jasusi wako,

Evarist Chahali

TANGAZO: unakaribishwa kujipatia machapisho yangu katika duka hili la mtandoni la vitabu vyangu (online bookshop) ambapo malipo yanafanyika kwa shilingi ya Tanzania (TZS). Duka hilo linapatikana hapa Duka La Chahali