Uchaguzi Mkuu wa Uingereza: Anguko la Conservatives na funzo kwa CCM, ushindi wa Labour na funzo kwa Chadema, ACT-Wazalendo
Juzi Julai 4, Waingereza walipiga kura katika uchaguzi mkuu ulioishia kwa chama tawala Conservatives kubwagwa vibaya na kulichokuwa chama kikuu cha upinzani cha Labour.
Na kutokana na matokeo hayo, aliyekuwa Waziri Mkuu na kiongozi wa Conservatives, Rishi Sunak, alijiuzulu jana, na kiongozi mkuu wa Labour, Sie Keir Stumer kurithi nafasi hiyo ya Uwaziri Mkuu.