Uchaguzi 2020: Membe Hawezi Kuwa Rais

Pamoja Na Taarifa Ya Mabadiliko Makubwa Kwa Kijarida Hiki

Samahani kwa kuchelewa kukutumia ktoleo la wiki hii la kijarida hiki.

Katika toleo la wiki iliyopita niligusia kidogo kuhusu “mchezo wa kuigiza” ambapo makada wawili wa CCM - Rostam na Membe “waliwashiana moto” hadharani kuhusu nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Nilieleza kuwa lengo la “maigizo” hayo ni “kumzuga” Jiwe Magufuli, ambapo kwa upande mmoja Jiwe anategenezewa mazingira ya kumuon Rostam kama BFF wake, na kwa upande mwingine Membe aonekane kama tishio kwelikweli ilhali mpinzani halisi anafichwa.

Kwa bahati mbaya - au nzuri - Jiwe “ameshaingia kichwakichwa” katika malengo yote mawili. Kwa sasa, Rostam ni BFF haswa. Ni mmoja wa watu muhimu wa Jiwe kwa muda huu, na ataendelea kuwa hivyo kwa muda mrefu. Lakini urafiki huu utkuwa na mwisho mbaya kwa Jiwe, kwa sababu there is only one winner, and it’s not him. Tuliache hilo kwa sasa.

Kwa upande wa Membe, Jiwe anaamini kwa dhati kuwa ndio mwana-CCM tishio kubwa kabisa kwake muda huu. Situation ipo complicated kwa kiasi flani japo panic ya Jiwe haina mashiko.

Membe ndio mtu aliyemfikisha Kipilimba - Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa - alipo leo. Membe na Kipilimba ni damu damu.

Naomba kabla ya kwenda kina zaidi niweke wazo angalizo hili muhumu: kitambo sasa Membe amekuwa “akiniandama” kwa minajili ya “kumsaidia” swahiba wake Kipilimba. Yeye Membe anajua kuwa ninajua, kama ambavyo Kipilimba anajua kuwa ninajua. Wanahangaika kwelikweli lakini nawamudu. Good news is, hawa wote ni kama “njiwa wangu. Sihitaji manati kwa ajili yao.” Siku moja huenda nitafafanua ninamaanisha nini.

Uswahiba wa Membe na Kipilimba unamuweka Jiwe kwenye wakati mgumu. Kitambo sasa Jiwe anatamani sana kumtoa Kipilimba lakini hana uwezo huo. Huyu “mchungaji” amemshika Jiwe kama mateka wake. Kuna u-freemason humo, ushirikina, na ukweli kwamba Kipilimba alimsaidia Jiwe kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kuiba kura pale Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambapo Kipilimba alipelekwa pale kwa kazi moja tu - kumwezesha mgombea urais wa CCM ashinde urais. And it worked.

Kila linalotokea kati ya Jiwe na Kipilimba linamfikia Membe, na nadhani hii inampa Membe matumaini ya urais. Ukweli mchungu ni kwamba hana nafasi hiyo. Sio kwa sababu hana sifa za urais bali ni mwanasiasa dhaifu aambaye licha ya kubebwa na Jk mwaka 2015 aliishia kufanya vibaya kwenye ndoto yake ya kuukwaa urais wa nchi yetu.

Let’s be honest: kama alishindwa kutumia mbeleko ya JK, ambaye alilazimika kumtosa swahiba wake Lowassa na kumuunga mkono Membe, ataweaje sasa ambapo kwa tunaofahamu undani wa siasa za Tanzania tunamuona ni “damaged goods”?

Of course I don’t like this guy (kwa sababu zangu binafsi) lakini hapa siongei kama mtu ninayemchukia bali natanabaisha ukweli mtupu: Membe hawezi kuwa rais no matter what. Hana sifa hata moja ya kuwa rais, na ni rahisi mno kubomolewa na wapinzani wake kwa sababu ana “mawaa” kibao. Huenda siku moja nikaeleza kuhusu “mawaa” hayo.

Yawezekana kabisa kuwa hata Membe mwenyewe anafahamu kuwa hana uwezo wa kuwa rais ila anatumika tu kama “chui wa karatasi” kumtisha jiwe.

Nakutakia siku na wiki njema

Ndimi mtumishi wako

Evarist Chahali