Ubalozi Wa Marekani Wasema Hospitali Dar Zimeelemewa Na Wagonjwa Wa Korona

Naomba kutafsiri sehemu ya taarifa husika.

Serikali ya Tanzania haijatoa taarifa zozote kuhusu UVIKO-19 (Ugonjwa wa Virusi vya Korona vya mwaka 2019) tangu Aprili 29 mwaka huu, kwahiyo hakuna takwimu zilizopo kuhusu idadi ya wenye maambukizo ya ugonjwa huo.

Uwezekano wa kuambikizwa ugonjwa huo jijini Dar es Salaam upo juu mno. Licha ya taarifa kiduchu, kila dalili yaonyesha kuwa ugonjwa huo unasambaa kwa kasi Dar es Salaam na sehemu nyingine nchini Tanzania.

Hospitali nyingi jijini Dar es Salaam zimeelemewa na wagonjwa wa UVIKO-19.