Twita imepata mmiliki mpya, tajiri namba moja duniani Elon Musk. Je hatua hii itakuathiri vipi wewe mtumiaji wa "Twita ya wa-Tanzania"?
Miongoni mwa habari kubwa zilizotawala wiki hii ni mtu tajiri kuliko wote, Elon Musk, kuwa mmiliki mpya wa mtandao wa kijamii wa Twita. Hatua hiyo imekuja baada ya sintofahamu iliyodumu miezi kadhaa.
Makala hii ni maalum kwako mtumiaji wa “Twita ya Watanzania”. Kwa minajili ya makala hii “Twita ya Watanzania” inamaanisha Watanzania wanaotumia Twita popot…