Twajua Magufuli Ni Dikteta Kamili. Tusichojua CDM, ACT Wana Mkakati Gani Kumng'oa

Kwa mara nyingine, jana Magufuli ameonyesha tena rangi yake halisi kuwa ni mtawala dikteta asiyeona aibu kukandamiza demokrasia na haki za binadamu.

Kwa upande mmoja, kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe alikamatwa kwa “kosa la kufanya mkutano halali wa ndani wa chama hicho” huko Lindi.

Kosa la Zitto ni kufanya kilekile ambacho ni halali kwa Makamu wa Rais Mama Samia

Image

Kwa upande mwingine, gazeti pekee lililosalia kama “sauti ya upinzani,” la Tanzania Daima, lilifutiwa leseni yake na serikali. Kwamba gazeti hili lingefungiwa lilikuwa suala la lini na sio kama (when not if)

Image

Kosa la gazeti hilo ni kuchapisha habari kuhusu Askofu Benson Bagonza, PhD, kuwataka Watanzania kudai haki zao

Image

Sidhani kama kuna mtu anayefuatilia japo kidogo siasa za Tanzania atakuwa ameshtushwa na tukio la kukamatwa kwa Zitto na Tanzania Daima kufutiwa leseni. Haya yamekuwa matukio ya kawaida katika miaka mitano ya utawala wa Magufuli.

Kwamba Magufuli ni dikteta, hilo halina mjadala. Vyama vya upinzani wa kweli, yaani Chadema na ACT-Wazalendo wanafahamu vema kuhusu hilo. Na Watanzania wanajua kuhusu hilo.

Lakini wasichojua Watanzania hao - nami nikiwa mmoja wao - ni nini vyama hivyo viwili vinapanga kufanya kukomesha udikteta wa Magufuli.

Moja ya nyenzo ambazo zingeweza kusaidia japo kidogo ni kwa Chadema na ACT-Wazalendo kuunganisha nguvu kwenye uchaguzi mkuu ujao. Lakini yaelekea kuwa ndoto hiyo imeyeyuka. Na katika hili wa kulaumiwa ni Chadema kwani Zitto na ACT-Wazalendo kwa ujumla wamekuwa wakifanya jitihada kubwa kutaka ushirikiano kwa vyama hivyo, lakini Chadema wameonyesha kutohitaji ushirikiano huo.

Lakini hata kama kila chama kimeamua kufanya mambo yake kivyake, bado tatizo li[o pale pale kuwa vyama hivyo havina clue kuhusu namna gani wanaweza kuzuwia udikteta wa Magufuli.

Ofkoz, mazingira ni magumu kwa vyama hivyo lakini si magumu kulinganisha na ilivyokuwa wakati wa mkoloni. Wala si ngumu kulinganisha na hali ilivyokuwa Afrika Kusini wakati wa Ukaburu.

Majuzi nilimsikia Zitto akidai kuwa wamejipanga vilivyo kukabiliana na jithada za Magufuli kurudia aliyofanya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Akadai kuwa wamekuwa wakiwasiliana na jumuiya ya kimataifa kuhusu yanayoendelea Tanzania. Nikabaki mdomo wazi. Jumuiya ya kimataifa hii hii iliyosamehe deni kwa Magufuli kutokana na “alivyoishughulikia vema korona.” Huu ni mzaha unaokera, kwa sababu jumuiya hiyo ya kimataifa inafahamu vizuri sana alichofanya Magufuli kwa watu wake.

Kwahiyo kuitegemea jumiya ya kimataifa ni kupoteza muda. Jumuiya ya kimataifa ipo wapi wakati Wapalestina wanafanyiwa unyama kwenye ardhi yao na Waisraeli? Jumuiya ya kimataifa ilikuwa wapi hadi kusubiri korona imwondoe Nkurunzinza aliyeua maelfu kwa maelfu ya wananchi wake? Na jumuiya ya kimataifa iko wapi wakati huu Dikteta Paul Biya anaangamiza maelfu ya Wakameruni wanaodai haki ya kujitawala?

Baadaye nikakutana na tamko hili la Chadema

Ni wazi kuwa hawa ndugu zetu aidha wanategemea miujiza ya kumfanya Magufuli abadilike mwenyewe au labda wameridhika na haya wanayofanyiwa, maana kuna dhana kwamba “udikteta wa Magufuli umwesaidia kuficha udhaifu wa baadhi ya vyama vya upinzani.”

Kwanini Askofu Bagonza apate ujasiri wa kutaka Watanzania wachukue hatua lakini si Mbowe au Zitto au Chadema au ACT-Wazalendo?

Image

Kuna wanaoweza kutetea kuwa “wakithubutu kutoa wito kama huo watakamatwa.” Hoja hiyo ni fyongo kwa sababu hata wasipofanya kosa wanaishia kukamatwa. Je isingekuwa motisha kwa wao kuamua “ you know what, hata tukikaa kimya tutaendelea kuonewa. Basi bora tupige kelele ili hata wakituonea basi angalau tumefanya kitu flani.”

Ikumbukwe pia katika miaka hii mitano ya udikteta wa Magufuli, sio Chadema au ACT-Wazalendo waliojaribu kufanya jaribio la kumtikisa dikteta huyo bali Mange ambaye japo maandamano yake hayakufanikiwa lakini aliwahenyesha polisi nchi nzima.

Naomba isitafsiriwe kuwa siwahurumii wapinzani. Na wala isidhaniwe kuwa nawashawishi wahamasishe vurugu. Hapana. Nachopigia mstari hapa ni kile kilichowahi kuongelewa na Dkt Slaa mwaka 2015 alipojiweka kando baada ya ujio wa Lowassa, ambapo alisema “mabadiliko ya kweli yataletwa kwa programu thabiti za mabadiliko zitakazohusisha watu wenye nia thabiti ya kuleta mabadiliko.”

Sina shaka hata chembe kuhusu both Mbowe na Zitto kwenye nia yao kuleta mabadiliko0 lakini what is lacking ni programu dhabiti ya kuleta mabadiliko hayo. Na bila hilo, itakuwa kama unatoka nyumbani na kuingia mtaani bila kuwa na idea unakwenda wapi. Chances are utaishia kupotea.

Ndimi jasusi wako

Evarist Chahali