Tuongee kidogo

Pengine “makala” hii itakuwaza kama wewe ni mlengwa, lakini ukweli una tabia moja kuu - kutouongea hakuufanyi uwe uongo.

Jana nilikuwa napitia takwimu za idadi ya wanaofungua baruapepe ninazowatumia vijarida. Kwa kweli takwimu zinavunja moyo mno.

Idadi ya mliojisajili mwanzoni ilikuwa zaidi ya watu 2,000. Baada ya kuwatumia baruapepe mara 10 nikafanya tathmini ya nani anafungua baruapepe nazomtumia, nani hafungui. Guess what, katika hao 2,000+ zaidi ya 800 walikuwa hawana muda wa kufungua baruapepe hizo. Nikawafuta.

Ndio nikaja na wazo la uanachama wa kulipia (paid subscription). Hili nalo halijawa na ufanisi kwa kweli. So far, mliojiunga kuwa paid subscribers ni kama 50 tu kati ya watu 1,300 hivi mliojiandikisha kuwa wanachama wa kulipia.

Of course, kuna wengi wenu mliotuma ujumbe kuwa hamna uwezo wa kulipia, na kwa vile lengo langu ni kuwatumikia na si kutengeneza faida, nikasikiliza vilio vyenu. Only for some kuendelea kutojali kufungua baruapepe zenye vijarida.

Kuna wengine mliomba niwavutie subira hadi mwisho wa mwezi, kisha wengine mkaomba japo wiki, nikatoa wiki mbili zaidi hadi Julai 14, 2019 lakini so far naona tunapotezeana muda.

Kwahiyo na chukua maamuzi magumu. Kuanzia wiki ijayo nitawatumikia ninyi 50 hivi mlioona umuhimu wa kuwa wanachama wa #BaruaYaChahali. In fact, siwatendei haki maana baadhi yenu, mlio nje ya Tanzania mmelipia USD 50 kwa mwaka, ilhali kuna mtu sio tu hana muda wa kuchangia bali pia analeta pozi kufungua vijarida anavyotumiwa.

Nafahamu kuwa kuwatumikia Watanzania sio kazi rahisi. Lakini tukiendelea kubembelezana kama watoto hatutoweza kuona mabadiliko. Ni bora niwatumikie watu wachache wenye uhitaji wa dhati wa vijarida hivi kuliko lundo la wazushi wanaoongeza tu idadi ya subscribers ilhali hawana muda wa kusoma.

Bado nitawatumia nyote kijarida cha #MtuHatari hapo kesho japo kitakuwa cha mwisho kwa ambao hamjajiunga na uanachama. Ikumbukwe kuwa idea ya uanachama ililenga kuondoa tatizo linalovunja moyo la mie kujituma kuwatumia vijarida lakini wengi wenu hamvisomi. Nikadhani kuwa mtu akilipia, atahamasika kusoma.

Anyway, niwatakie wikiendi njema. Samahani kwa nitakayekuwa nimemkwaza lakini kama kweli tunataka mabadiliko ni lazima tuambiane ukweli.

Ndimi mtumishi,

Evarist Chahali