Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu Atikisa Mahakama Kuu, Afichua Serikali Kufoji Nyaraka Kuhusu Mwenendo Wa Kesi Hiyo
🌐 Muhtasari
Jana 8 Septemba 2025, Mahakama Kuu ya Tanzania (Masjala Kuu, Dar es Salaam) ilisikiliza kesi ya awali ya Mh. Tundu Lissu, anayekabiliwa na shtaka la uhaini chini ya Kesi ya Jinai Na. 19605/2025. Hii ni kesi ya tatu tu ya uhaini katika historia ya Tanzania, baada ya zile za mwaka 1970 na 1983.
Licha ya kuwa mahabusu kwa siku 153, Lissu alifika mapema mahakamani huku akipokelewa na umati mkubwa wa wafuasi, viongozi wa upinzani, mabalozi wa kigeni, na mawakili zaidi ya 50. Serikali ilipiga marufuku waandishi wa habari kurekodi na pia ikakataza matumizi ya simu mahakamani kwa "usalama".
Makala hii iliyotafsiriwa kutoka lugha ya Kiingereza kutoka kijarida-dada cha Ujasusi Blog inakueleza kila unachohitaji kufahamu kuhusu mwenendo wa kesi hiyo hapo jana na mustakabali wake huko mbeleni