[#TumiaVPN]: Unakaribishwa Kujiunga Chaneli Yangu Ya YOUTUBE, Nimekuandalia Tathmini Ya Dk 6 Tu Ya Mwenendo wa Kampeni za JPM,Lissu,Membe,Dkt Mwinyi Na Maalim Seif

Baada ya kupokea ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali, nimeonelea ni vema “kuhuisha” chaneli yangu ya YouTube ambayo niliianzisha mwaka 2017 ila ni kama “niliitelekeza.”

Tafadhali angalia “video hii ya kwanza baada ya uzinduzi mpya wa chaneli”

Kisha kama hutojali, muunge mkono mtumishi/jasusi/kocha wako kwa ku-like video hiyo na ku-subscribe chaneli hiyo HAPA (Faida ya ku-subscribe ni kwamba “utashtuliwa” kila video mpya itakapobandikwa kwenye chaneli)

Katika mazingira ya sheria kandamizi dhidi ya haki yenu ya msingi ya kuhabarishwa, ni muhimu sie wadau wa haki za kijamii kuchukua hatua kama hizi ili hata wenye mamlaka wakizuwia vyombo vya habari vya huko nyumbani, sie tunaowajali huku nje tutaendelea kuhakikisha mnahabarishwa.

Pia nina furaha kuwatangazia wabunifu wote kuwa chaneli hiyo inapokea video za matukio muhimu kwa jamii, na mtuma video husika atalipwa stahili zake. Wasiliana nami HAPA

Licha ya video, pia ninakaribisha habari na makala -again zenye maslahi kwa jamii - na ikichapishwa kwenye gazeti la mtandaoni la HABARI TANZANIA basi mhusika atalipwa.

Uwe na wikiendi njema.

Ndimi mtumishi/jasusi/kocha wako,

Evarist Chahali