[#TumiaVPN: 'Mwanaharakati Huru' Musiba Amchimba Mkwara @MagufuliJP, Aonya Endapo Jina Lake Litakatwa Kamati Kuu

Cyprian Musiba, mmoja wa “wapigadebe” mahiri wa Rais Magufuli, anayejiita “mwanaharakati huru,” na ambaye anawania kupata ridhaa ya CCM kuwania ubunge wa jimbo la Mwibara ametuma ujumbe mkali kwa mwenyekiti wa taifa wa chama hicho na Kamati Kuu yake.

Katika ujumbe wa twiti ambayo aliandika kisha akaifuta, Musiba ambaye amekuwa mstari wa mbele kuwachafua watu mbalimbali anaodai ni wapinzani dhidi ya Rais Magufuli, amemuonya kiongozi huyo kuwa endapo jina lake halitopitishwa basi “patachimbika.”

Baadhi ya wana-CCM sio tu wanaona hatua hiyo kama dharau ya waziwazi ya “mpambe” huyo kwa Rais, bali pia wanatafsiri vitisho hivyo kama kumfanya Rais mateka wa kisiasa, kwamba “kila kada aliyemtetea Rais basi apewe upendeleo maalum.”

Musiba, ambaye pia ni mmiliki wa magazeti kadhaa, amewatahadharisha pia Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru, na Mwenezi, Humphrey Polepole, kuwa anafahamu “wamepanga kumhujumu, na ole wao kwani yeye si saizi yao.”

Habari hii ni endelevu.

Nimalizie kwa tangazo